Kasi ya intaneti inaongezeka duniani kote. Je unajua ni mataifa gani yanaongoza kwa uwepo wa huduma za intaneti zenye kasi zaidi? Marekani ata haionekani katika nafasi ya juu
Kampuni ya Akamai, inayomiliki mfumo unaotumiwa na tovuti mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha kasi na kiwango bora zaidi katika kustream video na miziki imetoa data zinazoonesha ubora wa kasi za intaneti kwa kipindi cha mwanzo wa mwaka huu.
Data zao zinaonesha wastani wa kasi ya intaneti imeongezeka takribani asilimia 12 ukilinganisha na kipindi cha mwisho wa mwaka 2015. Wastani wa kasi ya intaneti kufikia mwanzoni mwa mwaka huu ni Mbps 6.3. Wakati huo huo kwa kipindi cha mwaka mzima wa 2015 ukilinganisha na wastani wa kasi ya intaneti kwa mwaka 2016 basi kuna ukuaji wa asilimia 23%
Nani ni bingwa duniani katika kasi ya huduma ya intaneti?
Korea Kusini ndio nchi inayoongoza kwa kasi ya intaneti. Wastani wao wa huduma hiyo ni Mbps 29.0 – huu ukiwa ni ukuaji wa asilimia 8.6 ukilinganisha kipindi cha mwisho wa 2015.
Nafasi ya pili inashikiliwa na Norway kwa kasi ya Mbps 21.3, nafasi ya tatu inashikiliwa na Sweden kwa kasi ya Mbps 20.6
Marekani inashikilia nafasi ya 16 ikiwa na wastani wa kasi ya Mbps 15.3, ukuaji wa asilimia 7.7 kutoka mwishoni mwa mwaka 2015.
Ripoti hiyo haikuonesha wastani wa kasi ya intaneti kwa Tanzania ila ilionesha wastani wa muda unaochukua kufungua ukurasa mmoja wa tovuti ambapo katika orodha ya nchi kazaa za Afrika Tanzania ilikuwa moja ya nchi za chini kabisa. 3 kutoka mwisho, huku Kenya ikifanya vizuri kiasi, ikiwa kati kati.
Kwenye intaneti ya simu, kufungua ukurasa mmoja wa mtandao inachukua wastani wa sekunde 5.9, wakati pale intaneti ya broadband inapotumika inachukua wastani wa sekunde 5.8.
Unaweza shusha (PDF) na kusoma ripoti hiyo hapa – Mtandao wa Akamai