Kampuni inajulikna kama Nothing, hii ni kampuni mpya kabisa na inajihusisha na uzalishaji wa vifaa vya kielektroniki.
Kwa sasa wanajipanga ili mwezi julai waweze kuzindua simu yao ya kwanza, pengine jina la simu hiyo likawa Nothing Phone 1 au Nothing 1.

Ikumbukwe kwamba mwanzilishi wa kampuni hii bwana Carl Pei ni mmoja kati ya waanzilishi wa kampuni ya OnePlus.
Uzinduzi huu utakuwa wa aina yake na utakua unaruka moja kwa moja kupitia huduma ya ‘Live Stream’ na uzinduzi huu umepewa jina la la Nothing (Event).
Lakini hichi sio kifaa cha kwanza cha kampuni hii kukitoa, mwaka jana kampuni hii ilitoa spika za masikio ambazo hazina waya.

Ukaichana na hayo kampuni inasema kuwa bado ina mambo mengi sana ambayo inategemea kuja nayo ombi lao kubwa ni kwamba soko liwapokee tuu.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unaona kampuni za simu zinavyozidi ni vizuri na je kufanikiwa kwao katika soko kukoje? Au unahisi kufeli kwao ni rahisi sana?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.