fbpx

simu, Tecno, Uchambuzi

Ifahamu Kamera Ya TECNO Camon 15!

kamera-ya-tecno-camon-15

Sambaza

TECNO kama kawadia yao, wamekuja na kingine kipya, mara hii wamekuja na simu mpya ya TECNO Camon 15. Inajulikana wazi kuwa simu zao za matoleo ya camon zimejikita sana katika teknolojia ya picha.

Simu inakuja na kamera nne (4) ni simu chache sana sasa hivi ambazo zinakuja katika mfumo huu wa kamera. Najua una shauku ya kutaka kujua mfumo wa kamera wa simu hizo, leo TeknoKona tunakufahamisha kuhusiana na  hilo.

Kamera Kuu: mfumo wa kamera nne huku kamera kuu ikiwa na MP 48, Kamera mbili zikiwa na MP 2  , na ya nne ikiwa na lenzi ya  QVGA.  Mfumo huu pia unasapoti kurekodi video zenye ubora wa 1080p ambayo ni fremu 30 kwa sekunde.

Kamera Ya Mbele: MP 16 ikiwa ndani ya kioo cha LCD. Kwa teknolojia ya sasa ni kawaida kabisa kwani kwa sasa simu nyingi zinakuja huku kamera yake ikiwa ndani ya kioo.

INAYOHUSIANA  Airtel yakanusha madai ya kuondoka Kenya
TECNO camon 15
TECNO camon 15

Ukiachana na  ukubwa katika swala zima la megapixels katika simu hii bado kamera zake zinaweza fanya mambo mengi sana ukilinganisha na kamera za simu zingine.

 

Vilevile, kuna teknolojia ya kwanza kabisa kutoka TECNO ambayo inaweza kupiga picha katika mazingira ya giza kali tuu bila kutoa flash na picha ikatoka na mwanga wa kutosha (fikiria kupiga picha usiku wa manane) vile vile kamera ina vitu kibao kama vile AI (Artificial Intelligence) katika kamera yake.

INAYOHUSIANA  Samsung yaweka rekodi kwa kupata faida ya mamilioni ya dola ndani ya siku moja

Tazama Video Hii Kujionea Vipengele vyote katika kamera ya Camon 15

Tupe maoni yako hapo chini. Je, ulimwengu wa picha na kamera kwa ujumla umebadilishwa kupitia simu hii? ningepeda kusikia kutoka kwako. Usisahau kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kwa habari kede kede za teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com