fbpx
Intaneti, Kamera, Teknolojia, Usalama

Kamera ya kuangalia mambo ya kiusalama isiyohitaji kuchajiwa kwa mwaka mzima

kamera-ya-kuangalia-mambo-ya-kiusalama

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Kamera ni mlinzi namba moja au mbili kwa wengi baada ya askari anayelinda eneo husika lakini kadri miaka inavyosogea nayo teknolojia inazidi kupanuka. Kamera ya EverCam huenda ikavutia makampuni/mashirika mengi tu kuzinunua.

Ukweli ni kwamba matumizi ya kamera za kiusalama siku hizi yameendelea kuongezeka kwani watu wanaona umuhimu wa kuweka kamera majumbani mwao, ofisini, kwenye kumbi za starehe, n.k ili kuwa na jicho la pili ambalo utaweza kujua kinachoendelea hata kama wewe mwenyewe haupo eneo husika kwa muda huo.

EverCam ni kamera ambayo haitahitaji gharama kubwa kuweza kuiendesha kwa sababu ni ya kisasa zaidi isiyokuwa na maelekezo mengi kuweza kujua jinsi ya kuitumia.

Kwanini EverCam ni nzuri kwa mwenendo wa teknolojia hivi sasa?

 Unaweza kuipachika popote na haiingii maji.

Kamera nyingi tu za majumbani maofisini, majumbani, n.k zinafungwa sehemu kwa usaidizi wa kitu fulani ili zisiweze kudondoka na kuweza kupata matatizo, EverCam haina haja ya kufungwa, yenyewe inagusanishwa tu sehemu ambayo unataka kuiweka; ina sumaku za ndani kwa ndani inayoifanya kuweza kukaa sehemu yoyote itakapowekwa. Hata hivyo, ina sehemu maalum ya kuifunga na nut iwapo utahitaji kufanya hivyo.

INAYOHUSIANA  Samsung Wakuletea Diski ya TB 1 SSD Inayotosha Kiganjani

Mvua inaweza kuwa kikwazo kwa baadhi ya kamera lakini waliotengeneza kamera ya EverCam, Eufy wameweka kuifanya kamera hii isiwekeze kuingia na maji kabisa na kuendelea kufanya kazi kama kawaida.

mambo ya kiusalama
Kamera ya EverCam ina rekodi video za katika ubora wa 1080p za kiwango cha juu sana hata kama mvua inainyenyshea.

Haitumii waya.

Wakati kamera nyingi tunazifahamu zinakuwa zimeunganishwa na waya, kwenye EverCam hutatumia waya hata mmoja ili iweze kufanya kazi; inatumia teknolojia ya wireless na hivyo kufanya kile ambacho kimekusudiwa bila kuunganisha waya; ni kama kwenye kompyuta mtu anavyoweza kupata huduma ya intaneti bila kutumia modem au kuunganisha waya wa intaneti.

Uwezo wa kukaa na chaji.

Kipengele hiki kwa maoni yangu huenda ndio kitotu cha kuifanya kamera hii kuweza kuuzika sana kwani betri yake inapochajiwa mara moja basi haitahitaji tena kuchajiwa kwa muda mwa mwaka mmoja (siku 365 katika mwaka 🙄 🙄 ) au miaka mitatu ikiwa katika standby mode. Betri yake aina ya Lithium-ion ina 13400mAh.

Ubora wa picha na utendaji wake wa kazi.

EverCam ina vipuri vya kuweza kuhisi (sensor) aina ya Sony Exmor IMX 323. Kamera yenyewe inaweza kuzunguka kwa upana wa pembe nyuzi 140. Vilevile, kifaa hiki kinapeleka taarifa fupi (notifications) kwa mtu kulingana na alivyoainishwa kwenye mfumo wa kamera na hii haijalishi aina ya kitu ambacho inatoa taarifa.

INAYOHUSIANA  Leseni za WhatsApp Kenya: Wamiliki makundi ya WhatsApp watakiwa kuwa na Leseni
mambo ya kiusalama
EverCam inaweza kutambua sura za watu, wanyama au vitu mbalimbali na hivyo kuweza kuchambua kutorekodi kitu ambacho inakifahamu.

Diski uhifadhi na usalama wake

Huwenda ulifikiri kuwa hata kama kamera hii ina memori kadi basi itakuwa haina ulinzi, la hasha! Kwanza cha kufahamu EverCam ina diski uhifadhi yenye ukubwa wa GB 16 ambayo ina teknolojia ya AES 128-bit encryption kuweza kuondoa kabla ya kuona kilichomo kwenye memori kadi iwapo tu imechomekwa kwenye mashine yake tu wala ila baada ya kutolewa ulinzi inaweza kuunganishwa na kwenye simu/kompyuta hivyo mtu kuweza kuona kilichomo.

INAYOHUSIANA  Apple Energy: Apple Kujikita Katika Teknolojia Ya Nishati!

EverCam ina uwezo wa kutunza video ya mpaka mwaka mmoja pia mtumiaji wa kamera hiyo anaweza akawa analipia $2.99 kuweza kupata huduma ya kuhifadhi video hizo “Hewani” kwa usalama zaidi.

Bei yake na mengineyo

Kamera moja ni $219|Tsh. 492,750 na iwapo utahitaji kamera mbili itakugharimu $329|Tsh. 740,250 (bei zote zilizoainishwa ni za ughaibuni). EverCam inaruhusu kuweza kuiunganisha na programu tumishi ili kuona kinachoendelea wakati wowote na katika masasisho yatakayoletwa kwenye kamera hizo kupipia programu wezeshi itaruhusu vitu kama Alexa, Google Assistant.

mambo ya kiusalama
Vitu vinaunda EverCam; kamera rahisi unayoweza kuiweka popote pale kwa ajili ya kuwa jicho lako la pili.

Kamera ya EverCam ndio hiyo rumeichambua kwa kina, tunaakribisha maoni yako hapo chini kuhusu kifaa hiki muhimu kwa usalama wa mali zako.

Vyanzo: Gadgets 360, Engadget

Facebook Comments

Sambaza
2 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

2 Comments

  1. Kamera ya kuangalia mambo ya kiusalama isiyohitaji kuchajiwa kwa mwaka mzima – TeknoKona Teknolojia Tanzania
    April 21, 2018 at 5:48 pm

    […] post Kamera ya kuangalia mambo ya kiusalama isiyohitaji kuchajiwa kwa mwaka mzima appeared first on TeknoKona Teknolojia […]

  2. Jinsi gani Uchina inavyotumia kompyuta na kamera kuwakamata wahalifu
    April 23, 2018 at 5:50 pm

    […] Kamera ya kuangalia mambo ya kiusalama isiyohitaji kuchajiwa kwa mwaka mzima […]