fbpx

Jumia na skendo ya kudanganya data kwa wawekezaji! Yakanusha!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kampuni ya Jumia imejikuta katika skendo inayohusisha udanganyifu wa data za kimapato na wateja ikiwa ni takbribani mwezi mmoja tokea kampuni hiyo ianze kuuza hisa zake katika soko la hisa nchini Marekani.

Kampuni ya Jumia iliorodheshwa katika soko la hisa la New York (Wall Street) huku ikichukua sifa nyingi – wawekezaji wakiipatia jina la utani la ‘Africa’s Amazon’, yaani Amazon ya Afrika. Ukiwa na mlinganisho na kampuni kubwa ya Marekani ya Amazon inayotoa huduma zinazofanana na Jumia, ikiunganisha wauzaji mbalimbali na wanunuaji bidhaa.

Bei ya hisa zake imeporoka kwa takribani asilimia 15 baada ya madai ya Citron kuwekwa wazi.

Jumia na skendo ya kudanganya data  jumia hisa

Jumia na skendo ya kudanganya data: Tokea zianze kuuzwa rasmi April 12, skendo hii imeathiri sana, ila tayari kuna dalili ya kupanda tena kama wataweza kuwahakikishia wawekezaji dhidi ya madai ya Citron (Chanzo Yahoo)

 

Habari nzuri zimeanza kugeuka mbaya baada ya shirika moja la data linalofuatiliwa na wawekezaji la Citron kutoa ripoti likisema kampuni ya Jumia imedanganya kwenye data za ukuaji wake na wateja wake ili kuwavutia wawekezaji.

INAYOHUSIANA  Tumia WhatsApp kwenye Kompyuta Yako Sasa

Madai ya Citron;

  • Jumia wameripoti idadi kubwa ya watumiaji kuliko uhalisia – ikiwa ni mlinganisho wa idadi iliyokuwa kwenye moja ya ripoti ya Jumia kwa wawekezaji wake wakuu (kabla ya kuingia kwenye mfumo wa hisa)
    • Hisa za Jumia hazina thamani na kwamba wawekezaji wake watapata hasara tuu

Majibu ya Jumia;

jumia

Sancha, Mmoja wa wakurugenzi na waanzilishi wa kampuni ya Jumia

Sacha Poignonnec mmoja wa waanzilishi wa kampuni hiyo apinga vikali

  • Jumia imesema data za utumiaji wa huduma hiyo walizozitoa ni sahihi na hawatabadilisha
  • Ripoti hii ya Citron ni ya nia mbaya – kwani haina ukweli wowote bali inalenga kutengeneza wasiwasi kwa wawekezaji
    • Jumia wamesema utofauti wa namba unaweza ukawa ni wa kitofauti kulingana na muda na walengwa wa ripoti husika.
INAYOHUSIANA  Fahamu Kuhusu ShuleDirect na Harakati zao ktk Kusaidia Elimu Tanzania - Mahojiano na Faraja Nyalandu

Andrew Left wa Citron amekaririwa na chombo cha habari cha FT akisema anakaribisha Jumia waende kutoa malalamiko ya kisheria kwani atakuwa mwenye furaha kwenda kushindana nao kupitia ofisi ya usimamizi wa biashara za hisa ya Marekani.

Kama hufahamu ni kwamba kampuni ya Jumia inafanya kazi katika mataifa 14 barani Afrika, bado ipo katika kipindi cha uwekezaji na hivyo haitengenezi faida sana na hivyo inategemea wawekezaji wake katika kuhakikisha inakuwa na kuweza kutengeneza faida miaka ya baadae.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.