Mwasisi wa mtandao wa kufichua maovu duniani Wikileaks, Julian Assange amekamatwa jijini London baada ya kuishi ndani ya ubalozi wa Ecuado nchini Uingereza kwa miaka saba.
Karibu miaka saba iliyopita Bw. Assange alikimbilia ubalozi wa Ecuador kwenye ardhi ya Uingereza akikwepa kupelekwa nchini Sweden kwa makosa ya ubakaji lakini mashitaka hayo baadae yalifutwa.
Mwazilishi huyo mwenza wa WikiLeaks ni raia wa Sweden, alikuwa akiishi ndani ya ubalozi wa Ecuador-Uingereza kwa karibu miaka saba iliyopita lakini sasa yupo mikononi mwa sheria tangu Aprili 11 2019 akikabiliwa na shitaka moja nchini Uingereza na mengine kadhaa kwa Marekani.
Kwanini Ecuador imeacha kumpa hifadhi?
Tangu aingie madarakani rais mpya wa Ecuador, Mhe. Lenin Moreno alishaweka wazi kuwa hadhani kama ataweza kuendelea kumwekea kinga Bw. Assange lakini kubwa zaidi ambalo lilikera ni pale mwezi Januari 2019 mtandao wa WikiLeaks ulipoweka wazi nyaraka ambazo hazifai kuonekana kwa watu kuhusu Vatican na kuaminika kuwa amehusika na sakata hilo, kuzuia kamera za ubalozini wakati alipokuwa akitembelewa na familia yake, kuweza kupata kuona nyaraka mbalimbali kwenye ubalozi huo na hata kugombana na walinzi ndani ya alipokuwa amepewa hifadhi.
Marekani pia inamtaka Bw. Assange
Mwaka 2006, mtandao wa WikiLeaks ndio ulianzishwa na miaka minne baadae (2010) mtandao huo kwa ushirikiano na Afisa wa zamani kitengo cha intelijensia, Bi. Chelsea Manning aliyeweza kupakua kanzi data ziptazo nne kati ya mwezi Januari na Mei 2010 kisha kuwapa WikiLeaks kwa msaada wa kutoa nenosiri ili kuweza kuona taarifa mbalimbali kuhusu idara ya ulinzi na usalama ya Marekani ingawa haifahamiki kama zoezi hilo la kudukua nenosiri lilifanikiwa au la!
Mwaka 2010, WikiLeaks ilitoa picha ikiwaonyesha wanajeshi wa Marekani wakiwapiga risasi wananchi kutoka kwenye helikopta nchini Iraq. Bi. Manning aliachishwa kazi, akasomewa mashitaka na kukutwa na hatia lakini huku yake ilipunguzwa na kupewa kifungo kingine kwani alikuwa anakabiliwa na kesi ya kunyongwa hadi kufa.
Adhabu zinazomkabili mwazilishi mweza wa WikiLeaks
Polisi waliporuhusiwa kuingia ndani ya ubalozi wa Ecuador, saa moja baadae Bw. Assange alfikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka akapatikana na hatia kwa kosa la kukimbia na kutofika mahakamani mwaka 2012 na anakabiliwa na kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa hilo.
Kwa kesi iliyokuwa ikimkabili wakati huo. Kwa kosa la kusirikiana na Bi. Manning kuweza kuwa na uwezo wa kuona itu ndani ya kazi data anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka mitano jela. Lakini kuhusu kupelekwa Marekani, serikali ya Uingereza ilikubali kwa maandishi kuwa hawatampeleka huko (Marekani) ambako anaweza akabiliwa na adhabu ya kuteswa au hukumu ya kifo.