fbpx

Afya, Maujanja, simu

Jinsi ya Kusafisha Simu yako

jinsi-ya-kusafisha-simu-yako

Sambaza

Je unafahamu jinsi ya kusafisha simu yako? Tukiwa katika janga la Coronavirus ni muhimu sana kuepuka kujishika uso, lakini je unafahamu jinsi ya kuhakikisha kitu kinachogusa kichwa chako mara kadhaa kwa siku ni kisafi?

Kitengo cha Serikali ya Marekani kinachoshugulikia masuala la milipuko ya magonjwa (Centers for Disease Control and Prevention) kinatambua simu kama moja ya kitu kinachoweza kusambaza virusi kwa urahisi.

simu na coronavirus
Jinsi ya Kusafisha Simu: Ni kipindi ambacho simu inatumika sana kupata taarifa zaidi kuhusu Coronavirus; lakini je tunahakikisha simu zetu ni safi?

Kumbuka;

  • Simu huwa unaiweka sehemu mbalimbali kama meza n.k.
  • Pia ukisalimiana au kushika vitu mbalimbali mwisho wa siku huwa unashika simu yako
  • Pia katika kuongea na simu kwa kuileta kichwani basi tunawapa virusi nafasi kulifikia eneo la uso kwa urahisi
INAYOHUSIANA  Utoaji wa talaka kwa njia ya simu wakemewa

Muhimu kuepuka;

Kumbuka simu nyingi hazina uwezo wa kuepusha maeneo ya ndani kulowa na maji, hivyo epuka suala la uoshaji wa kutumia maji mengi.

Pia kuna vitu ambavyo havifai kabisa kutumika katika usafishaji wa simu kwani vinaweza kuharibu kioo/display ya simu. Epuka vimiminika vya kusafishia vyenye kemikali kali, mfano sabuni za kusafishia mikono (hand sanitisers), ‘bleach’, chochote chenye kemikali za ‘chroline’ au bidhaa za kusafishia vioo vya magari au madirisha.

Jambo la kufanya.

> Njia ya kwanza

Vitambaa laini vinavyouzwa kwenye maduka ya dawa (‘Wipes’) zenye uwezo wa kuua vijidudu vinafaa kutumika. Hivi huwa havina unyevunyevu mwingi na hivyo ni salama kutumika. Unaweza kutumia hivi na baada ya hapo ukatumia kitu kikavu kama vile ‘toilet paper’ au kitambaa kingine ambacho unauhakika kipo salama.

INAYOHUSIANA  Rwanda yapiga marufuku matumizi ya simu kwa wanafunzi shuleni

> Njia ya pili

Kutumia sabuni ya kawaida ya kuogea yenye sifa na uwezo wa kuua virusi na bakteria, kama vile Dettol na zingine za jamii kama hii.

Changanya sabuni na maji kidogo. Chukua kitambaa laini kama leso au vile vitambaa vya kusafishia miwani. Kilainishe kidogo na kisha safisha simu yako katika maeneo yote ya nje kwa utaratibu, usitumie nguvu za kusugua – si muhimu.

Muhimu kufahamu:

  • Ni muhimu uzime simu yako kabla ya kuanza kuisafisha.
  • Epuka kutumia maji/maji mengi. Ni simu chache hasa hasa za bei ya juu ndio zinauwezo wa kuhimili kuloweshwa na maji mengi/yanayotiririka.
  • Hakikisha simu imekauka vizuri kabla ya kuiwasha tena.
INAYOHUSIANA  Facebook: Kubadilisha nywila (nenosiri) inawezekana!
coronavirus simu safisha simu
Endelea kufuata taratibu za usafi kama unavyoshauriwa na Wizara ya Afya

Kumbuka kusambaza makala hii kwa ndugu na marafiki katika kipindi hichi tunachopambana na janga la Coronavirus. Kumbuka, makala hii inaongelea suala la usafi wa simu yako pekee, katika kipindi hicho hicho hakikisha unafuata ushauri kutoka Wizara ya Afya hasa hasa katika kuhakikisha unanawa mara kwa mara. Kumbuka simu safi itakuhitaji na wewe pia kuhakikisha una mikono misafi mara zote.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |