Hivi katika pita pita zako katika mitandao ya kijamii haujawahi kukutana na maneno ambayo yamegeuka yaani yanaonekana kama yamepinduka hivi (chini juu).
Kama ulishawahi na hujua namna ya kufanya au hujawahi basi hapa uko sehemu sahihi. Kwa kutaka sifa kabisa ngoja nkusalimie kwanza, ¡¡ɐuoʞouʞǝ┴ nqᴉɹɐʞ ¿oʞɐ⅄ ᴉɹɐqɐH
Haya ngoja niache sifa, kwa kifupi ni kwamba kuna njia nyingi ambazo unaweza kuzitumia kuweza kufanya zoezi hili ila kwa leo ntakuaonyesha hii moja tuu ingawa kuna mitandao mingi inaweza ikawezesha zoezi hili
3. Fliptext.net
Kwa kutumia njia ya kwanza ya Upsidedowntext.com ni kwamba unaweza ukageuza maneno yakawa chini juu katika simu za Android, iOs , Windows na hata katika kompyuta yako.
Kwa kutumia kifaa chako ingia katika mtandao wa www.Upsidedowntext.com/ na ukifanikiwa utaona vimetokea viboksi viwili
Kile cha juu utaweza kuandika neno ambalo unataka lionekane chini juu, neno hilo litaonekana chini juu katika kiboksi kingine cha pale chini.
Baada ya neno kutokea pale chini likiwa limeshageuka chini juu basi unaweza ukalinakili (copy) na kisha ukaenda kuli’paste’ katika mtandao wa kijamii.
Najua ukitumia njia hii unaweza ukapa maswali mengi sana, watu wanaweza wakakuuliza kuwa umewezaje kufanya hivyo. Kitu kizuri ni kutokuwa mchoyo waambie TeknoKona wamekujuza.