Tunaweza kupoteza vifaa vyetu vya kielektroniki, pia vinaweza kuibiwa, je tunavipata vipi? Kama uwezekano wa kuvipata unashindikana, je, tunaweza futa taarifa zetu nyeti?
Kwa dunia ya sasa ni mara chache sana watu wanaumia kuhusu kifaa ukilinganisha na taarifa za ndani ya kifaa pindi tuu kifaa kinapoibiwa au kupotea.
Tumeshaandika sana kuhusu jinsi ya kuipata simu kama ikiwa imeibwa au kupotea na pia jinsi ya kufuta taarifa katika simu hiyo.
Unaweza Kusoma Zaidi Kuhusiana Na Hilo Katika Simu >>HAPA<< na >>HAPA<<
Vipi Kuhusu Laptop ya Windows?

Ndio unaweza kufuta taarifa katika laptop yako, lakini lazima laptop hiyo iwe inatumia programu endeshi kutoka windows (itapenda kama ikiwa ni toleo la juu kabisa).
Cha kwanza kabisa (kabla ya yote) ili kuwezesha hili ni lazima uwe una uhakika kuwa sehemu ya ‘Find My Device” (tafuta kifaa changu) imewashwa katika laptop hiyo.
• Hakikisha Ume ‘Sign in’ kwa kutumia akaunti yako ya Microsoft katika laptop hiyo.
• Kama unatumia Windows 10, nenda Settings > Update & Security > Find my device na hakikisha kipengele kimewashwa.
• Kama Windows 11, nenda Settings > Privacy & security > Find my device na hakikisha kipengele kimewashwa.
Mpaka hapo umefikia nusu ya kuliwezesha hili, haya tuendelee…
Sasa unatakiwa katika Laptop yako uwe na Microsoft Intune, hii ni programu ya kimtandao ambayo inaweza kukusaidia kusimamia vifaa vyako na baadhi ya App (Hakina tofauti kubwa na Find My Phone).
Pakia katika Laptop yako kutoka katika Microsoft Store au unaweza ku’Sign in’ kwenye Company Portal website.
Mpaka hapo, sasa kama Laptop yako itakua imepotea au kuibwa unaweza ukafuata vitu bila ya kuwa nayo.
• Nenda katika portal.azure.com/#home na kisha ingia kwa kutumia akaunti yako.
• Chagua All Services na kisha Intune.
• Chagua Microsoft Intune na kisha chagua Devices.
• Chagua kifaa ambacho ambacho kimepotea/kimeibwa (Unachotaka kufuta taarifa).
• Chagua Wipe na kisha kubali kwa kubofya Yes.
• Kama Laptop yako iliyopotea/kuibwa ikiwasha, taarifa zako zitafutwa ndani ya dakika 15.
Mpaka hapo utaku umewezesha hili, pindi laptop yako inapo ibwa/kupotea unaweza ukatumia njia hii kufuta taarifa — Cha msingi kukumbuka hapa ni kwamba lazima Laptop iwe inatumia Windows.

Ningependa Kusikia Kutoka Kwako, Je Wewe Ni Mmoja Wapo Kati Ya Wale Ambao Ni Wahanga Wa Kupotelewa Na Laptop?, Niandikie Hapo chini Katika Eneo La Comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.