Ni mara nyingi sana watu kuanzisha jina katika mitandao ya kijamii au majukwaa mengine lakini baadae wakataka badilisha jina hilo.
Kuna baadhi ya majukwa hayaruhusu kubadilisha majina hayo ya utambuzi. Kwa upande wa Youtube wao wana njia yao ya kukusaidia katika hili.

Tumeshawahi kuona wasanii wengi kuwa na jina moja na baadae kubadilisha tena na kuwa na jingine, saa fikiria kama msanii huyo katika mtandao huo wa youtube kama asingeweza kubadilisha jina hilo la mwanzo.
Fuata Njia Hizi Ili Kuliwezesha Hilo!
Nenda katika eneo la menu ndani ya studio ya Youtube, kasha ingina katika “Custumization” na kisha ingia katika ‘Basic Info”

Ukiwa humo ndani ndio unaweza kabisa kubadilisha jina la chaneli yako ndani ya huo mtandao
Ukimaliza hapo basi chagua ‘publish’ ili kumaliza, hapo jina litakua limebadilika.
Njia hiyo hapo juu ni kwa kutumia kompyuta, lakini hata kwa simu unaweza kubadilisha jina hilo la chaneli huko Youtube.

Kama ni mtumiaji wa Android au hata ukiwa mtumiaji wa iPhone fungua App yako ya Youtube na kisha chagua my channel na kisha ingia katika eneo la kuhariri (edit).. hapo unaweza badilisha chaneli yako.
Mpaka nadhani unaweza badilisha jina la chaneli yako katika mtandao wa Youtube
Niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hili umelipokeaje?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.