Unaweza ukawa unatumia kompyuta ambayo kihifadhi data hakijagawanywa. Je, unajua kuwa ni hatari kutumia kompyuta ambayo diski huifadhi haijagawanywa? Pata kufahamu kutoka kwetu, TeknoKona.
Ni muhimu sana kuhakikisha kuwa kompyuta unayotumia hard disk yake imegawanywa na hili kuweza kugawanya hard disk (HDD) ya kompyuta yako ni muhimu kufuata hatua zifuatazo:-
- Fungua Disk Management kwenye komyuta. Kwa urahisi unaweza kufungua kwa kutumia ‘Run‘ (bonyeza kitufe cha ‘Windows+R‘) kisha andika ‘diskmgmt.msc‘.
Ukurasa wa Disk Mangement; sehemu mahususi inayowezesha kugawanya kihifadhi data kwa urahisi. - Bonyeza sehemu iliyoandikwa “Unallocated” (ina ufito mweusi) kisha chagua New Volume ili kuweza kutengeneza partition mpya kwenye HardDisk. Pia kama diski nzima ni Drive C na unaona bado ina nafasi nyingi ambayo inaweza ikatosha kuwa nafasi mpya basi ichague kisha bofya Shrink.
‘Right click’ sehemu yenye ufito mweusi kisha chagua New simple Volume. - Weka kiasi ambacho unataka partition unayoitengeneza kwenye kihifadhi data kwenye kompyuta yako kiwe nacho. Kisha bonyeza Next.
Weka kiasi ambacho unataka kihifadhi data iwe nacho kwenye partition mpya. - Chagua herufi ambayo unataka partition yake iwe nayo. Inaweza kuwa herufi E, F, H lakini sio herufi C kisha bonyeza Next.
Chagua herufi yoyote unayotaka partition unayoitengeneza iitwe lakini isiwe C. - Unaweza kuchagua kufuta (format) kila kitu kwenye ile sehemu ya hard disk unayoitengeneza. Kufuta chagua ya pili katika orodha na kama hutaki kufuta kila kitu basi chagua ya kwanza katika orodha halafu bonyeza Next.
Ukichagua ya pili katika orodha tambua kuwa kila kitu kwenye partition unayoitengeneza vitafutika. - Bonyeza Next kuweza kumaliza mchakato mzima wa kugawanya kihifadhi data katika kompyuta yako. Kisha bonyeza Finish kama ishara ya kukamilisha mchakato mzima wa kutengenza parttion.
Maelezo ya kina kuhusu partition ambayo unakaribia kumaliza kuitengeneza.
Kwa hatua hizo kwa hakika utakuwa umewza kuigawanya diski uhifadhi na kutokana na maombi ya wasomaji wetu, kutaka kujua jinsi ya kuigawanya kihifadhi data, TeknoKona imeitika ombi na imewajuza.
Imeandikwa kwa kutokana na ujuzi binafsi pamoja na picha kutoka TechNet Magazine