fbpx
Apple, IPhone, simu, Teknolojia

iPhone SE 2020 imetoka baada ya fununu nyingi

iphone-se-2020-imetoka-baada-ya-fununu-nyingi
Sambaza

Baada ya fununu za kutosha tuu kuhusu iPhone SE 2020 ama kwa lugha nyingine toleo la pili kwa mtangulizi wake Apple wameona inafaa kuizindua simu hiyo ambayo inaendana na teknolojia ambayo ipo kwenye umaarufu wake.

Kwa karibu mwaka mmoja sasa palikuwepo na tetesi kuhusu ujio wa iPhone SE 2020 ambayo kimsingi inafanana sana na iPhone 8 lakini pamoja na hayo pia imeboreshwa kipuri mama, memori. Fuata nami kuweza kufahamu mengi zaidi:

Kioo/Muonekano

Kama nilivyokwisha kusema kwenye maelezo yangu ya utangulizi simu hii inafanana kabisa na iPhone 8 kwa muonekano huku urefu wa kioo chake ukiwa ni inchi 4.7 (750*1334px) ambacho ni LCD.

INAYOHUSIANA  Je umeshawahi tumia poda ya JOHNSON'S !? Ina skendo ya kusababisha kansa ya kizazi!

Kamera/Usalama

Uwezo wa kamera kwenye simu husika ni MP 12 kwa kamera ya nyuma (kuu)+flash, MP 7 kwa ile ya mbele. Apple wameweka teknolojia ya kutumia kidole (touch ID) kama sehemu ya kuifanya rununu hiyo iwe na ulinzi.

iPhone SE 2020
iPhone SE toleo la 2020.

Kipuri mama/Betri

Moja ya kitu ambacho kinachangia ufanisi bora wa simu janja ni aina ya kiini cha kifa husika hapa namaanisha “Kipuri mama”; kwenye iPhone SE toleo jipya imewekwa A13 Bionic ikiwa ndio teknolojia ya kisasa kabisa kutoka familia ya vipuri vinavyotengenzwa na Apple. Nguvu ya betri ni 1821mAh sawa na kwenye iPhone 8.

INAYOHUSIANA  Verily, kuja na viatu vyenye uwezo wa kumpima mvaaji uzito

Memori/Mengineyo

Apple wameboresha kipengele cha memori mahususi kabisa kwenye RAM ambapo mtiririko wake ni 64GB 3GB RAM, 128GB 3GB RAM, 256GB 3GB RAM. Bei yake inaanzia $399|zaidi ya Tsh. 917,700, GB 128 ni $449|zaidi ya Tsh. 1,032,700  (ile ya GB 256 ni $549|zaidi ya Tsh. 1,262,700) kwa bei ya ughaibuni, haina sehemu ya kuchomeka spika za masikioni, inakuja ikiwa na iOS 13, ina Gigabit-class LTE ambayo ni kasi zaidi kuliko LTE iliyozoeleka, pia inatumia eSIM, inatumia Bluetooth 5, inaweza kutoingia maji umbali wa kina cha mita moja kwa mpaka dakika thelathini (30).

INAYOHUSIANA  iPhone Ikiwa Inaendeshwa Na OS Ya Android!

iPhone SE 2020

Simu hiyo inatazamiwa kuingia sokkoni wiki ya mwisho wa mwezi Aprili na wengi wakiitazama kama “Pacha” wake iPhone 8 kutokana na kuwa sifa sawa kwenye vipengele mbalimbali.

Vyanzo: MacRumors, GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|