iPhone ni moja kati ya simu janja zenye kamera nzuri sana, licha ya kamera zake kusifika kwa kupiga picha kali bado inasemekana kuanzia toleo la iPhone 15 Pro na kuendelea watakuja na teknolojia ya periscope.

Teknolojia ya Periscope katika lensi ya kamera huwa inakua imejikita kabisa katika swala zimu la kuvuta (zoom) kwa ubora wa hali ya juu hata kama kinachopigwa picha kitakua mbali.
https://twitter.com/mingchikuo/status/1547456847309045760
Mwaka huu tunazisubiria kwa hamu sana simu za iPhone 14 ambazo kwa kiasi kikubwa zitakua na maboresho kadha wa kadha katika eneo la kamera

Licha ya maboresho hayo lakini teknolojia ya periscope kwenye simu hizo (iphone 14) haitakuwepo kabisa kwenye vifaa hivyo
Hata baadhi ya iPhone 15 pia hazitakuwa na kipengele hichi labda kuanzia toleo la iPhone 15 Pro na matoleo mengine baada ya hapo.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini kwenye uwanja wa comment je hili umelipokeaje? Unadhani ni sawa kwa simu hii kuja nateknolojia hii? Je ina tija?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.