fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android apps instagram iOS

Instagram: Uwezo wa kuficha idadi ya waliopenda kwenye chapisho husika

Instagram: Uwezo wa kuficha idadi ya waliopenda kwenye chapisho husika

Spread the love

Instagram ambayo hivi sasa inasifika kwa kuumpa mtumiaji uwezo wa kuchagua kuficha idadi ya watu waliopenda/waliotazama chapisho husika sasa imeboreshwa tena!.

Kipengele kipya cha kumpa uhuru mtumiaji wa Instagram kupitia simu janja kwamba anao uwezo wa kuficha watu wangapi wametokea kupenda kile alichokipandisha. Sasa wahusika wameamua kutanua wigo.

chapisho husika

Kipengele kipya kwenye Instagram: Uwezo wa kuficha idadi ya watu waliotazama/kupenda ulichokiweka.

Instagram imenogesha kipengele hicho cha kuficha idadi ya watu wliopenda chapisho kwa kumuwezesha mtumiaji kuamua ni lipi la kuonyesha au kuficha; waundaji wampa anayetumia programu tumishi kuficha idadi ya waliopenda/waliotazama chapisho husika.

Faida za kipengele cha kuficha idadi ya watu waliopenda chapisho husika kwenye Instagram

Umaarufu wa chapisho unatoa tafsiri kwamba kile ulichokiweka kimewavutia watu wengi hivyo kinaweza kuwa kama chanzo cha mapato. Lakini tukiangalia upande wa pili wa shilingi unapoamua kuficha unakuwa unaelekeza umakini kwenye kile ulichokiweka na si idadi ya waliovutiwa nacho kwani kuna uwezekano mkuwa wa kufedheka iwapo chapisho husika halitapokelewa vizuri.

chapisho husika

Instagram yaboreshwa kwa kuruhusu mtumiaji kuweza kuficha idadi ya watu waliopenda kwenye kilichowekwa.

Kipengele hiki kipya kimepokelewa kwa mtazamo tofauti lakini mwisho wa siku wewe ndio mwenye kuamua kuficha ama la!Tunakaribisha maoni yako kuhusu hili au kitu kingine. Daima tunasema usiache kutufuatilia kila uchwao.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania