fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

instagram Mtandao wa Kijamii

Instagram Kuja Na Stika Ya ‘Reshare!

Instagram Kuja Na Stika Ya ‘Reshare!

Spread the love

Ni wazi kwamba mtandao wa kijamii wa Instagram unazidi kukuwa kila siku na kila siku kuna vipengele vingi inaviongeza ili kuhakikisha kuwa inazidi kusonga mbele.

Kipengele cha Reshare ndio kipya kabisa na hichi kitasaadia sana sana katika kuhakikisha kuwa una’post post ya mtu kwa kupitia sehemu ya story.

Kipengele Cha Reshare Katika Mtandao Wa Instagram

Kipengele Cha Reshare Katika Mtandao Wa Instagram

Yaani kipengele hiki kitakua kinafanya kazi kwa kuangaliza post zote ambazo umeziona ndani ya lisaa na kuziita “recently viewed”.

Sasa basi kipengele cha “recently viewed” kitatokea baada ya kuingia katika kipengele cha ‘Reshare’ na hapo unaweza ukachagua cha kushare na marafiki zako.

Kumbuka kwa mara ya kwanza kama ulikua unataka kufanya hivyo ilibidi kwanza uende katika post husika na kisha ndio uweze kuisambaza katika story yako.

SOMA PIA  Facebook kuzuia akaunti Feki

Kipengele hichi kinavuyoangaliwa ni kwamba kitafanya watu wajifikirie zaidi pale wanapotaka kusambaza kitu katika story zao.

Ningependa Kusikia Kutoka Kwako, Niandikie Hapo Chini Katika Eneo La Comment, Hii Umeipokeaje?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe  Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania