fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps instagram Intaneti Mtandao wa Kijamii Teknolojia

Instagram inafanya Majaribio ya kuweka Vikumbusho kwenye jukwaa lake

Instagram inafanya Majaribio ya kuweka Vikumbusho kwenye jukwaa lake
Spread the love

Mtandao wa kijamii wa Instagram umekuwa ukifanya maboresho ya huduma zake kupitia taarifa wanazopata kwenye tafiti mbalimbali wanazaofanya kuhusiana na matumizi ya jukwaa hilo. Hivi karibuni Mkuu wa Instagram Adam Mosseri ametangaza  kuwa kampuni hiyo imeanza kujaribu kipengele kipya wiki hii kiitwacho “Pumzika”.

Kitufe hicho ambacho kitaongezewa kitawawezesha watumiaji kupumzika kutumia programu ya Instagram. Kitufe hichi kitakuwa ni cha hiari kila mtu anauwezo wa kukitumia endapo ataamua na kitakuwa kinakukumbusha kila baada ya dakika 10, 20 au 30 kuwa upumzike kutumia programu ya Instagram.

Instagram inafanya Majaribio

Picha: Mtu akitumia Instagram

Uongozi wa Instagram ulisema pia kuwa kipengee hicho kipya hakitaadhiri ufanyaji kazi wa programu yao. Vikumbusho vipya vya “Pumzika” vinazinduliwa wiki hii kama jaribio na idadi ndogo ya watumiaji, kwa sasa, lakini kampuni inatarajia kusambaza kipengele hicho hadharani katika miezi ijayo.

SOMA PIA  Google wapigwa faini Ufaransa: Kulipa zaidi ya dola bilioni 1 za Kimarekani

Chanzo: Techcrunch

Endelea kutembelea tovuti yetu kufahamu zaidi kuhusu teknolojia na matumizi yake. Soma makala zetu zingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania