fbpx

Infinix ZERO 6 imekuja na Teknolojia Ya AI (Artificial Intelligence) Nchini! #Tanzania

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Baada ya uzinduzi rasmi wa Infinix  ZERO 6 nchini Tanzania, simu yenye teknolojia ya Artificial intelligence, wengi wamekuwa wakihoji kuhusiana na ufanyaji kazi wa teknolojia hiyo, hivyo basi leo ningependa kuwajuza namna teknolojia ya AI kwenye kamera za Infinix ZERO 6 inavyofanya kazi.

Pamoja na sifa zingine nzuri za infinix ZERO 6, sifa kuu zaidi ya Infinix ZERO 6 ni kamera, Infinix Zero 6 imewekwa nguvu nyingi sana upande wa kamera ambapo kamera za nyuma ni MP 12+MP 24 zenye kupiga picha/picha jongefu na mng’ao  wa hali ya juu sana, na kamera ya mbele ni MP 20.

Infinix ZERO 6

Na katika kuongeza ubora wa kamera ndipo teknolojia ya AI inapofanya kazi sambamba na kamera. Teknolojia ya AI inaiwezesha ZERO 6 kupiga picha zenye muonekano halisi ya mazingira husika mfano kama ni bahari au ua basi utapata picha zenye rangi halisi ya vitu hivyo.

INAYOHUSIANA  Redmi 7: Simu nzuri halafu kwa bei ya kawaida

Vilevile, kioo cha mbele kimewekewa ulinzi kwani ni kioo cha Gorilla chenye inchi 6.2. Uwezo wake wa betri ni 3650 mAh pamoja na XCharge kwa ajili ya teknolojia ya kuchaji haraka.

Infinix ZERO 6

Kijana kutoka Infinix akitoa maelezo juu ya teknolojia ya AI katika ZERO 6 inavyofanya kazi

Mbali na kamera, imekuwa ni kama tamaduni kwa Infinix kuzalisha simu zenye muonekano wa kuvutia na safari hii wanatupa asilimia 100% kwani wamehama kabisa kutoka material ya plastiki na chuma chepesi  hadi kwenye aluminum.

INAYOHUSIANA  Tetesi: Instagram Kuwekewa uwezo wa ku'chat'!

Infinix imezingatia swala la rangi, imekuja na rangi tatu tofauti Milan Black, Sapphire Cyan na Champagne Gold, simu hii inapatikana nchi nzima .

Sifa Za Infinix ZERO 6 Kwa Ufupi
Uwezo wa Mtandao: 4G/3G/2G
Toleo Endeshaji: AndroidTM 8.1
Kioo: 6.18 INCH FHD+
Prosesa: Qualcomm SDM 636
Ukubwa: 156.8*75.9*7.95mm
ROM + RAM: 64GB + 6GB
Ujazo Wa Betri: 3650mAh
Kamera Ya Mbele: 12MP AF+24MP AF Ikiwa Na Uwezo Wa Flash
Kamera  Ya Nyuma: 20MP 4IN1 Ikiwa na Uwezo Wa Flash
INAYOHUSIANA  BBM Yaja Na Maboresho Kabambe

Ningependa kusikia kutoka kwako, sifa hizi ukilinganisha na simu zingine kubwa kubwa unaona mapinduzi ya namna gani katika teknolojia za simu na makampuni ya simu kwa ujumla.

Kwa habari kama hizi na zingine nyingi kuhusiana na teknolojia usisite kutembelea mtandao wako pendwa wa teknokona kila siku kwani TeknoKona daima tupo na wewe katika teknolojia.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.