fbpx
Infinix, simu, Tanzania

Infinix S5 Pro: Infinix Kuja na Kitu Kipya Zaidi

infinix-s5-pro-infinix-kuja-na-kitu-kipya-zaidi
Sambaza

Kupitia ukurasa wao wa Instagram, kampuni ya simu za mkononi Infinix Mobile Tanzania wametoa tamko kwamba baada ya Infinix S5 sasa wanakuja na Infinix S5 Pro ikiwa ni muendelezo wenye maboresho.

Hata hivyo Infinix hawakutoa sifa za simu hio lakini inasemekana itakuja na Kamera inayotokeza kwa juu (Pop up Camera) na meboresho mengine hasa upande wa Kamera na ujazo (storage).

INAYOHUSIANA  Infinix Zero 5 Pro: Simu janja mpya yenye kukaa na chaji siku mbili
Infinix S5 Pro
Infinix S5 Pro: Baadhi ya picha za kuutangaza ujio huo. #Teaser

Hii ni moja ya Ishara kwamba Biashara bado zinaendelea japokuwa kuna ugonjwa uliotikisa dunia, COVID19. Ni matumaini ya makampuni mengi janga hili litaweza kupita ndani ya muda mfupi na mambo yakarudi kama kawaida.

Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, Infinix wamesisitiza wateja wao kuchukua tahadhari na kujikinga na maambukizi hayo hatari na pia wameweka mazingira salama katika maduka yao yote.

INAYOHUSIANA  Tuzo za TEHAMA zinazoratibiwa/kutolewa na TCRA

Simu inatarajiwa kutambulishwa rasmi katikati ya mwezi wa huu wa nne.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |