Taarifa ambazo zilikuwepo mwanzoni ni kwamba kampuni ya Apple ilikuwa na mpango wa kuweka huduma yake ya iMessage mpaka katika vifaa vya Android
Jambo hili lingekuwa ni la aina yake kwani linge ongeza idadi ya watumiaji wa iMessage na pia jinsi ya kuwasiliana kungezidi kuwa rahisi baina ya mtu na mtu
App wamesema wana sababu kadhaa ambazo zimefawafanya kukatisha mipango hiyo ya iMessage kwa sasa. Kumbuka kwa sasa watu wanashauku kubwa ya kuona hiyo iOS 10 itakuaje katika mikono yao maana vitu ambavyo Apple imetangaza kuwa itakuja navyo ni balaa tupu!
Kwa sasa vitu ambavyo vimeboresha na vinategemewa na watu ni iOS 10, MacOS Sierra na Siri kuwepo katika Mac zile za Desktop
Kampuni ya Apple ilitoa sababu mbili juu ya kwanini hakutakuwepo na iMessage katika vifaa vya Android kwa sasa
Sababu ya Kwanza: Apple tayari imekuwa kwa kiasi kikubwa sana – lakini wanaweza ongeza namba — kiasi cha kwamba wanafurahia sehemu ambayo wamefikia. Mpaka sasa wana watumiaji bilioni moja duniani kote ambao wanatumia vifaa vya Apple.
Sababu ya pili: Apple pia imekiri kuwa moja kati ya mpango wake ni kujitofautisha na wengine. Kumbuka Apple ina vitu kibao ambavyo inajitegemea yenyewe kama yenyewe na huwezi ukavikuta katika vifaa vingine kamwe.
Huduma ya iMessage kwa sasa inapatikana katika vifaa vya Apple peke yake. Kwa kufanya hivyo kampuni itaweza kuwavutia watu kujiunga (kwa kununua vifaa vyao) na kufurahia huduma zao – kama iMessage – tofauti wangesema kuwa huduma hiyo inapatikana katika Android kuna watu wangeenda nunua vifaa vya Android na kuwahama
Kwa kifupi Apple bado inaendelea na tabia yake ile ile ya kila siku ya kujitegemea na sijui kama watabadilika kwa kipindi chochote cha karibuni kinachokuja. Utofauti wao mpaka leo ndio unaolifanya kampuni kuwa moja kati ya makampuni makubwa duniani.
Niandikie hapo chini sehemu ya comment umepokea vipi usitisho huu? Kama wewe ni mtumiji wa Android/Apple niambie nini mtazamo wako kwa simu na vifaa vya Apple
Kwa habari za kiteknolojia na maujanja mbali mbali tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Hashiman (@hashdough) Nuh
Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com
One Comment
Comments are closed.