Baada ya sakata la Cambridge Analytica kuhusu mtandao wa Facebook kutumia taarifa za watumiaji wa mtandao huo wa kijamii; mbinu ya kuepukana na dhahama ya kudukuliwa kwa taarifa zako kwenye akaunti yako imebainishwa!
Katika akaunti ya Facebook kumekuwa na programu kadhaa zinazotembea pamoja na akaunti yako hivyo kuwepo na uwezekano mkubwa wa kudukuliwa kwa mawasiliano yako.
Facebook imetoa fursa kwa watumiaji wake kuweza kuziondoa programu hizo mara moja ambapo hapo awali hakukuwa na uwezekano wa kuweza kuzitoa programu hizo. Baadhi ya programu aidha umeziunganisha mwenyewe au hukuziunganisha mwenyewe lakini sasa unaweza kuziondoa zote kama una wasiwasi kwamba zinaweza kuwa chanzo cha kudukuliwa mawasiliano yako.
Baadhi ya akaunti unaweza kukuta hakuna hata programu moja iliyounganishwa katika akaunti husika hivyo ina maana upo safi wala hakuna haja ya lazima ukute progarmu.
Namna ya kuangalia na kuondosha programu zilizounganishwa na akaunti yako ya Facebook.
- Fungua tovuti ya Facebook kisha fungua akaunti yako. Nenda moja kwa moja kwenye settings,
- Kisha fungua Apps and Websites kisha utaona programu zilizounganishwa na akaunti yako (kama hakuna basi heri),
- Kama zipo weka alama ya ‘Pata‘ kwenye kila kiboksi na kisha bonyeza remove kuziondoa. Baada ya hapo utakuwa salama zaidi kuepuka programu ambazo zingeweza kudukua mawasiliano yako.

