fbpx

Ifahamu simu ya Nokia 5. #Uchambuzi

0

Sambaza

Nokia 5 ni simu yenye muonekano mzuri, na huku ikiwa na ubora mzuri tena kwa bei nafuu. Simu hii ilitambulishwa rasmi Februari mwaka 2017 na kampuni ya HMD Global.

Kwa undani fahamu; Makubaliano ya Nokia na HMD Global katika utengenezaji wa simu za Nokia.

Tokea HMD Global waanze kutengeneza simu za Nokia zinazotumia Android tayari jina hilo maarufu katika sekta ya simu za mawasiliano limeanza kurudi tena kwenye chati.

nokia 5 bei uchambuzi

Leo fahamu kwa undani sifa na uwezo wa simu simu hii.

Inaukubwa wa Inchi 5.2 na huku bodi lake likiwa limetengenezwa kwa kutumia alumini. Display/kioo chake ni cha Gorilla Glass na hivyo kinaweza kudumu kwa muda mrefu bila kuwa na mikwaruzo.

INAYOHUSIANA  Samsung Galaxy S10 kuwa na mfuko wa kuhifadhi sarafu za kidijiti

nokia 5

  • Ina uzito wa gramu 160 na unene wa milimita 8.
  • Display: HD 1280×720
  • Prosesa: Qualcomm Snapdragon 430
  • RAM: GB 2
  • Betri: mAh 3000
  • Android: Inakuja na toleo la Android 7.1.1 – ikiwa haijawekwa makolombwezo yoyote na Nokia.
  • Kamera: Ina kamera ya Megapixel 13 ikiwa na flash mbili.
  • Vinginevyo-Bluetooth 4.1, LTE 4G, na headphone jack ya kawaida. Uwezo wa laini mbili.

Ina uwezo wa kufunguliwa kwa kutumia alama za vidole (fingerprint sensor), na teknolojia hii imewekwa katika eneo la kubofya ‘Home’.

Simu ya Nokia 5 inapatikana katika rangi 4; Nyeusi, Bati, Bluu na Shaba.

nokia 5 nyeusi

Bei ya Nokia 5: Kutegemea na maduka kwa maduka Nokia 5 inapatikana kwa bei ya kati ya Tsh 490,000/= – Tsh 550,000/=.

INAYOHUSIANA  Amazon kuunda programu ya kujipima nguo

Ni simu nzuri kwa mtu mwenye bajeti ya kufikia 500,000 na huku akiitaji simu yenye ubora.

Je, ulishawahi kuiona au kutumia Nokia 5? Tupe maoni yako juu ya ubora wake?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.