fbpx

Hummingbad: Kirusi kilichoteketeza zaidi ya simu janja mil. 10

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kirusi hichi kinasemekana kuharibu simu janja zenye kutumia programu endeshaji maarufu ya Android na iOS(kwa mara ya kwanza), kimeharibu zaidi ya simu janja milioni 10 na zaidi.

Soma Pia – Je tunahitaji Anti-Virus katika simu za Android?

hunningbad

Kwa muujibu wa taarifa kutoka Check Point zinasema kuwa kirusi hicho kina uwezo wa kuathiri simu janja au tablet na kuweza kudukua taarifa mbalimbali muhimu kutoka kwenye barua pepe, taarifa zako za benki na kingine chochote kitakachohitajika ili kuweza kukamilisha uhalifu na kisha kuuza taarifa hizo kwa wezi wa mitandaoni.

Jinsi kirusi hicho kinavyoathiri simu janja/tablet zenye kutumia Android/iOS

Iwapo mtu atatembelea tovuti ambayo siyo ya kweli, kirusi hicho kitajaribu kuingia kwenye simu janja/tablet na kujaribu kupata ruhusa ya kufanya/kuona kila kitu (root access) na ikishindikana kirusi hicho kitajaribu kumuwezeshesha mtu kuweza kufanya karibu kila kitu kwenye tovuti aliyoitembelea mfano unapoambiwa ubonyeze linki fulani kuweza kuangalia video ya ngono.

INAYOHUSIANA  Wanaolipia Spotify wafikia milioni 100

Kama hayo yote mawili yakishindikana kirusi hicho kitatuma taarifa ya uwongo kukujulisha(notification) uweze ku-update simu janja/tablet yako na ukidanganyika na kuruhusu maboresho kufanyika(updating) basi kirusi hicho kitakuwa kimepata ruhusa ya kudukua taarifa zako na kuziuza kwa wezi.

Taarifa zinasema kuwa Uchina kirusi hicho kimeathiri sana vifaa ya kielekroniki(simu janja/tablet) kwa wingi zaidi, takribani vifaa 1.6m ikifuatiwa na India(1.35m), Marekani ikiwa nafasi ya tatu katika idadi ya simu janja/tablets  ikifuatiwa na Australia na Uingereza kwa pamoja jumla ya vifaa 100,000 vikiharibiwa na kirusi hicho.

hummingbad

Chati ikionyesha nchi zilizoathiriwa na kirusi hicho chenye kuathiri simu janja/tablet

Google wanasema kuwa wanataarifa kuhusu kirusi hicho na wamekuwa wakizuia apps zilizokwishaharibiwa na kirusi hicho kuweza kupakuliwa na kuboresha kompyuta zao ili kuweza kuufanya taarifa za wateja wao kuwa salama zaidi.

INAYOHUSIANA  Mambo yanayokera katika makundi ya WhatsApp

Iwapo kifaa chako kimeathiriwa na kirusi hiki jambo la kufanya ni kufuta kila kitu(restore factory) kwenye simu janja/tablet. Epuka kupakua app kutoka kwenye tovuti isiyoaminika(kama sio kutoka kwenye app store/apple store).

Teknokona inakushauri uwe makini pale unapokutana na mitandao au apps zisizoeleweka. Kuwa muangalifu, unashauriwa kupakua apps kutoka soko husika la apps katika simu yako tuu – kiusalama.

> Soma Pia – Je tunahitaji Anti-Virus katika simu za Android?

INAYOHUSIANA  Kuwa Makini App Za Bure Zinaweza Kuiba Data Zako!

> Simu ipo slow?? Fanya yafuatayo irudie kasi yake! #Maujanja

Endelea kufuatilia Teknokona kuweza kujua mengi zaidi kuhusu kirusi hiki.

Makala hii imeandikwa kwa usaidizi wa vyanzo kama theguardian, tech Times pamoja na vyanzo vingine mbalimbali.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.