Mamlaka ya maji safi na taka za mikoa mbalimbali ya Tanzania, zimesogeza huduma zake kwa wananchi wake kupitia simu za kiganjani.
Mamlaka hizo zimerahisisha huduma zao kwa kuziunganisha katika simu za mkononi ili mteja aweze kulipia ankara zake mbalimbali.
Pia huduma zingine ambazo mteja anaweza kuzipata kupitia simu ni kujua salio lake la kulipia huduma ya maji, kuripoti tatizo linalohusiana na huduma hiyo na mengine mengi yanayohusiana na huduma za maji.
Huduma hiyo mpaka sasa zimeunganishwa kwa mikoa sita ya Dodoma (DUWASA), Iringa (IRUWASA), Arusha (AUWSA), Mwanza (MWAUWASA), Tanga (TANGAUWASA) na Dar es Salaam (DAWASA).
Ili mteja aweze kupata huduma hizo atalazimika kufungua simu yake katika eneo la kupigia na kuingiza *152*00# ambapo itafunguka menu na atabofya nambari 6 (Maji) kisha utachagua jina la mamlaka ya maji kulingana na mkoa uliopo kati ya hiyo sita.