Mdundo ni huduma ya utirirshaji na upakuaji wa miziki ya kiafrika mtandaoni. Huduma hii ya mdundo inapatikana kupitia tovuti yake pamoja na app ya Mdundo. Mdundo ilianzishwa maalum kwaajili ya kuwasaidia wasanii wa kiafrika kuuza na kusambaza nyimbo zao katika bara zima la Afrika.
Hivi karibuni huduma hii ya utiririshaji wa muziki yenye makao makuu yake jijini Nairobi imetangaza kuwa jukwaa hilo lilirekodi watumiaji wa kipekee Milioni 16.4 kwa kipindi cha robo mwaka kilichoishia Septemba 2021, Huu ni ukuaji wa 10% ukilinganisha na robo ya awali.
Ukuaji huo ulichangiwa zaidi na ongezeko kubwa la watumiaji nchini Kenya, Tanzania na Afrika Kusini. Tanzania ilikuwa na watumiaji wengi zaidi katika robo ya mwaka huu, ikirekodi watumiaji wa kipekee Milioni 4.1, huku Nigeria na Kenya zikirekodi watumiaji Milioni 3.1 na Milioni 2.6.
Rachel Karanu, Mkuu wa Mdundo wa Biashara ya Ubia barani Afrika alisema kuwa “Ukuaji wa kasi katika maeneo yote unaonyesha kuwa jukwaa letu limegusa watumiaji na wateja wetu wa utangazaji katika Mdundo For Brands. Tunafanya kazi kwa ukaribu na mashirika maarufu yenye watumiaji Afrika nzima ili kuongeza ushawishi wa watumiaji, kwa hivyo ni habari njema kwamba tunaongeza ufikiaji wa chapa yetu na washirika wetu wa utangazaji. Tunatazamia robo ya mwisho ya mwaka ambapo tunatarajia kukuza zaidi ufikiaji wa jukwaa letu na pia kuongeza thamani kwa washirika wenzetutu wa chapa” Aliongeza.
Baadhi ya kampuni zilizofanya kazi na Mdundo nchini Kenya, Nigeria na Tanzania katika kipindi cha robo mwaka ni pamoja na Sportpesa, Safaricom, Chrome Gin, Standard Chartered Bank, Captain Morgan, Coca Cola, BetKing na Guinness Smooth.
Chanzo: Techmoran
No Comment! Be the first one.