fbpx

Huawei Wazalisha Simu Chache Zenye Chata La KFC Huko China!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kampuni ya Huawei ni moja kati ya makampuni makubwa sana duniani katika uzalishaji na uuzaji wa simu. Hivi karibuni kampuni hiyo imezalisha simu zake ambazo zinachata (logo) ya KFC.

Dhumuni kubwa la kuzalisha simu hizi ni kusheherekea maadhimisho ya miaka 30 ya huduma chakula cha haraka huko china.

Moja Ya Mgahawa Wa KFC Huko China

Huawei sio wa kwanza kutoa simu za muda kulingana na kitu fulani mara nyingi kampuni ya simu ya Samsung na yenyewe imeonekana ikifanya hivyo.

INAYOHUSIANA  BRELA: Usajili wa Kampuni na Biashara sasa kwa Mtandao

Kwa mfano kampuni ya Samsung ilitoa matoleo kama yale ya Samsung Galaxy S8 toleo la Pirates of the Caribbean , the Samsung Galaxy S7 toleo la Edge Injustice na Samsung Galaxy S6 Edge toleo la  Iron Man.

SImu Ya Huawei Enjoy 7 Plus — Toleo La KFC

Kwa Huawei hili ndio toleo lake la kwanza ambalo linabeba dhima ya kipekee kama matoleo hayo ya Samsung yalivyo.

INAYOHUSIANA  Ifahamu Program Endeshaji Mpya Ya Android Baada Ya 'Android Nougat!

KFC ilianzishwa miaka 30 iliyopta huko china, Mpaka sasa KFC ndio mgahawa mkubwa kuliko yote huko China ukiwa umeenea zaidi ya maeneo 5,000.

SIFA ZAKE
Jina la simu ni Huawei Enjoy 7 Plus toleo la KFC

Kioo chake ni Inchi 5.5  720p

Kamera ya MP 12

Prosesa ya Qualcomm Snapdragon 435

RAM GB 3

Ujazo wa uhifadhi GB 32

SImu Ya Huawei Enjoy 7 Plus — Toleo La KFC

Kampuni ya Huawei imetengeneza simu hizo 5000 tuu na simu hiyo ikinunuliwa inakuja na vitu kibao ndani ya App ya KFC.

INAYOHUSIANA  Ushindani katika vioo vinavyojikunja

Ni vigumu sana kuona simu hii imetoka nje ya China kwani imezalishwa kwa unit ndogo sana na dhima kubwa ya kutengenezwa ni kusheherekea miaka 30 ya chakula cha haraka. Lakini pengine inaweza ikaonekana katika masoko ya mtandaoni kama vile ebay na Amazon.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niambie hii umeipokeaje? je wewe binafsi unapenda simu kuleta matoleo ya aina yake kulingana na mambo ambayo yanatokea? niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuka Kutembelea TeknoKona Kila Siku Kwa Kuwa Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.