fbpx

CIA: Huawei Wanapokea Msaada Wa Kifedha Kutoka Mashirika Ya Ulinzi Na Usalama!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Huawei wanapokea msaada wa kifedha kutoka mashirika ya ulinzi na usalama ya China, haya ndio madai mapya yaliyotolewa na shirika la kijasusi la Marekani (CIA).

CIA wamedai kwa namna moja au nyingine Huawei imepokea fedha kwa ajili ya uwekezaji kutoka kwa mashirika makubwa yenye mizizi au mahusiano na vyombo vya usalama vya nchi hiyo.

Ukiachana na kuwa kampuni kubwa ya mawasiliano huko nchini china, kampuni hii bado inashikilia namba mbili — ambao  ipo katikati ya Apple na Samsung–  hili lilitokea baada ya Huwei kuipita Apple kiamuzo ya simu na kuchukua nafasi yake ya pili.

Huawei Wanapokea Msaada Wa Kifedha

Ni kwamba makampuni ambayo yanatoa fedha hizo moja kwa moja yanajihusisha na mambo ya usalama. Kwa upande wa CIA wameona ni vyema kuyaonya mataifa mengine mengi kama vile Australia, New Zealand na Canada.

INAYOHUSIANA  Hacker ahukumiwa kifungo cha miaka 4 kwa kosa la kudukua siri za Jeshi la Marekani

Kumbuka kampuni ya Huawei iko mbioni kuingia katika mkataba mkubwa na  Uingereza katika kuhakikisha kuwa Huawei inalisaidia taifa hilo katika kusasisha (Upgrade) teknolojia ya 5G katika mawasiliano.

CIA pia haikuishia hapo ilitaja wafadhili hao ambao ni sehemu ya jeshi (People’s Liberation Army), Tume ya usalama ya China (China’s National Security Commission) na tawi la mtandao wa kiintelejensia wa china (Chinese state intelligence network). Wametaja mashirika haya na kuwaweka wazi watu ambao wanafanya kazi na Huawei na dunia nzima kwa ujumla.

Kwa kifupi ni Kwamba CIA Imewatonya washkaji zake juu ya hili na kuwataka waliangalie kwa kina jambo hili

Kwanini CIA Wamefanya Hivi?

Tukiangazia katika swala zima la ulinzi na usalama, taarifa ndio kitu cha muhimu sana (zinaweza leta/kuvunja usalama). Kwa mataifa makubwa taarifa huwa zinapewa kipaumbele kikubwa na zinatunzwa sana.

INAYOHUSIANA  Tanesco kuja na makundi kwenye WhatsApp

Fikiria kama Huawei kwa mfano akawa kweli kapokea fedha katika makampuni hayo, hii inaonyesha ni moja kwa moja lazima makampuni hayo yataitumia Huawei kama chombo chake cha upelelezi na pia kukusanya taarifa za mataifa mbali mbali.

Wanasiasa wengi wamekua na mtazamo tofauti tofauti juu ya jambo hili na wengine wametaka kabisa kampuni hiyo ifungiwe (au ifungiwe kufanya kazi maeneo fulani). Kwa upande wao Huawei wamekataa na kusema kuwa hizo ni kashfa tuu kutoka kwa CIA ambazo hazina ukweli wowote.

INAYOHUSIANA  Uraibu wa kutumia kompyuta: Serikali ya Korea Kusini yapata suluhisho

Habari zingine juu ya sakata hili;

Kwa upande wangu naona hili ni jambo ambalo linaweza kuirudisha Huawei nyuma, ikumbukwe kua huawei ina biashara nyingi na mataifa mengi. Hili likibainika kuwa ni kweli basi kampuni itapoteza biashara nyingi.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini mtazamo wako juu ya hili. Kumbuka kutembelea TeknoKona kila siku kwani daima tupo nawe katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com