fbpx
Android, Honor, Huawei, simu, Uchambuzi

Huawei waendelea kutoa toleo jingine la simu za Honor

huawei-waendelea-kutoa-toleo-jingine-la-simu-za-honor
Sambaza

Huawei ndio wanaomiliki bidhaa zinazobeba jina la Honor na wameendelea kutoa simu janja kwa mwaka 2018 na kuifanya kuwa ya kiushindani kutokana na bidhaa yenyewe kuwa na mashiko.

Simu janja ambayo imezinduliwa kutoka Honor ni Honor 9i (2018) ambayo inaifanya bidhaa yenye na kampuni mama kuendelea kuwa washindani kwenye soko la simu janja.

Honor 9i ndio simu janja ya kwanza kuwa na kamera nne, kitu ambacho kwa wale ambao kupiga picha au video basi simu hii inakupa nafasi pana zaidi.

toleo jingine la simu
Honor 9i ambayo imeingia katika kumbukumbu kwa kuwa simu janja ya kwanza kuwa na kamera mbili mbili kila upande yaani ule wa nyuma pamoja na kwenye uso wa mbele.

Sifa ilizonazo Honor 9i

Simu hii imezinduliwa mwezi Juni 2018 na kwa mujibu wa tovuti mbalimbali imeonekana kupata maoni mazuri. Ina sifa zifuatazo:-

INAYOHUSIANA  Matangazo Ya Samsung Kuwa Vifaa Vya Kuchajia Galaxy S10!

Kioo: Kioo chake kina ukubwa wa inchi 5.84 lakini simu ni ya kitofauti kidogo kwani kioo chake kinaonekana chochote bila ya kuwa na vitu vingine juu yake (full display view).

Prosesa & Betri: Honor 9i ina octa-core HiSilicon Kirin 659 SoC na kile kinachofanya picha zionekane ang’avu (GPU) ni  Mali T830-MP2. Betri yake ina 3000 mAh.

Kamera & Programu endeshi: Kamera ya kwanza ya nyuma ina MP 13 na ya pembeni yake ina MP 2 pamoja na LED flash. Kamera za mbele ina MP 16 na kamera zote mbili zinakubali kuchukua picha jongefu katika kiwango cha 1080p.

toleo jingine la simu
Muonekano ang’avu wa Honor 9i inapatikana katika rangi Nyeusi, Bluu, Kijani na Zambarau.

Diski uhifadhi & RAM: Kwenye diski uhifadhi zipo Honor 9i za aina mbili; kuna zile zenye GB 64 na nyingine zina GB 128 huku zote zikiwa na uwezo wa kukubali uhifadhi wa ziada wa mpaka GB 256. RAM yake ni GB 4.

INAYOHUSIANA  Simu janja chini ya nusu ya asilimia moja ndio zinatumia Oreo #Ripoti

Kadi za simu & Sifa nyinginezo: Inatumia kadi mbili za simu na zote zikiwa ni zile za kukata (ndogo). Unaweza kutumia alama ya kidole/uso kuweza kufungua simu. Pia ina teknolojia ya 4G LTE, Wi-Fi 802.11ac, Bluetooth, GPS/ A-GPS, na Micro-USB.

toleo jingine la simu
Muonekano wa Honor 9i kwa nyuma; mfuniko wake ni wa chuma.

Upatikanaji wa Honor 9i kwa sasa ni kwa kuagiza kwani bei yake bado haijawekwa wazi ila ukiagiza ni zaidi ya $200 | Tsh. 460,000 (ya GB 64) na $261 (GB 128) | Tsh. 600,300.

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

1 Comments

  1. Huawei waendelea kutoa toleo jingine la simu za Honor – TeknoKona Teknolojia Tanzania
    June 15, 2018 at 4:30 pm

    […] post Huawei waendelea kutoa toleo jingine la simu za Honor appeared first on TeknoKona Teknolojia […]