fbpx
Android, apps, Huawei, Xiaomi

Huawei, Oppo, Vivo, na Xiaomi Kuungana Katika Kutengeneza Mbadala Wa Playstore!

huawei-na-wengine-kuja-na-soko-lao
Sambaza

Makampuni nguli kutoka China yaani  Huawei, Oppo, Vivo, na Xiaomi ambayo yapo vizuri katika teknolojia za utengenezaji wa simu janja, yameunganisha nguvu katika kuja na mbadala wa soko la apps la #Google PlayStore.

Mbadala huu unahusisha moja kwa moja soko maarufu zaidi duniani yaani Playstore kutoka Google. ukiachana na kuwa mbadala wa Google playstore bado kampuni imeweka wazi kuwa soko hili pia litakua mahususi kwa ajili ya kupunguza kero kwa wandaaji na wasambazaji wa Apps, muziki, video n.k.

INAYOHUSIANA  Android Marshmallow: Google Watangaza Jina La Toleo Jipya La Android
Huawei, Oppo, Vivo, and Xiaomi
Huawei, Oppo, Vivo, and Xiaomi

Hili linatokea lakini kumbuka simu zingine yaani Oppo, Vivo, na Xiaomi wao bado wana ruhusa ya kutumia Playstore kwa asilimia 100 ukiachana na wenzao wa Huawei ambao mwaka jana walipatwa na kashfa ya kiulinzi na kiusalama.

Huawei walijikita katika kutengeneza OS yake ili waachane na ile maarufu ya Android ambayo ndio maarufu zaidi na ambayo imewaletea vikwazo vingi katika soko la marekani.

Katie Williams, ambae ni mchambuzi katika Sensor Tower, amesema kuwa app za google ambazo zimazuiliwa china kwa mwaka jana zimetengeneza takribani dola za kimarekani  bilioni 8.8. duniani kote.

INAYOHUSIANA  Fahamu jinsi ya kukimbia foleni kwa kutumia Google Maps

Simu zote yaani  Huawei, Oppo, Vivo na Xiaomi zinachangia kwa asilimia  40.1 kwa simu janja zote zinazouzika duniani, hii ikiwa na maana kuwa asilimia iliyobakia pekee ndio inachokuliwa na simu zingine zilizobakia ukichanganya zile za Apple na samsung. Taarifa hizi ni kwa mwongo wa mwisho wa mwaka 2019.

Mbadala Wa Playstore Huawei, Oppo, Vivo, and Xiaomi
Huawei, Oppo, Vivo, and Xiaomi

Licha ya makampuni haya yote kuungana lakini bado haijawekwa wazi kuwa kampuni zote hizi zinachangia asilimia ngapi ili kuhakikisha zoezi hili linatimia.

INAYOHUSIANA  Pokemon Go: Gemu Tishio kwa mitandao ya kijamii

Teknokona tumelipokea vyema jambo hili, kumbuka hii ni njia moja wapo ya kuimarisha huduma na ushindani ukazidi kuongezeka katika masoko ya Apps. Vile vile kumbuka sio vizuri kumtegemea mtu mmoja katika biashara hivyo hii ni hatua nzuri zaidi kwa samsung.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya maoni. kumbuka kutembelea mtandao wako wa TeknoKona kila siku kwani daima tupo nawe katika teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com