fbpx

Huawei na simu ya kwanza yenye RAM GB 8

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Vita katika kuifanya simu janja iweze kufanya kazi vyema ndio kitu ambacho kinafanya makampuni mbalimbali kutoa simu ambazo zina RAM kubwa na hivyo kufanya kuvutia watu wengi.

Katika hali iilyowashangaza wengi Huawei kwa mara ia kwanza kabisa kupitia bidhaa ambayo inauzwa chini ya yake nikimaanisha Honor imetoa simu ambayo ina RAM yenye ukubwa wa GB 8; hakuna simu yoyote ya Huawei au Honor yenye RAM ya ukubwa huo, Honor 10 GT ndio ya kwanza.

Sifa za Honor 10 GT.

Ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja tu kupita tangu Honor 10 itoke Huawei wameleta toleo jingine ambalo lina tofauti ndogo na mtangulizi wake na hivyo ukizingalia kwa haraka haraka simu zote mbili inakuwa ni vigumu kubaini tofauti zao.

Kioo/Muonekano. Simu hii ina ukubwa wa kioo chenye inchi 5.8|uwiano wa 19:9 (2280 x 1080 LCD) na kimuonekano ni kama ule wa simu janja za karibuni; kuwa na sifa umbo la herufi V (notch) kwenye kioo na ile teknolojia ya usalama kwa kutumia kidole imewekwa kwenye kitufe cha nyumbani.

INAYOHUSIANA  Motorola RAZR ipo njiani kuja lakini kivingine

Prosesa. Honor wameendelea na mtindo wake uleule kama ilivyo kwenye Honor 10 kwa kutumia aina ileile ya prosesa yaani Kirin 970. Betri yake ina uwezo wa 3400mAh.

simu ya kwanza yenye RAM GB 8

Moja ya prosesa za kisasa zinazotumiwa kwenye simu janja za Huawei.

Kamera. Kwenye kamera ya mbele ina MP 24 mahususi kabisa kwa ajili ya selfie na kwa upande wa nyuma kuna kamera mbili; moja ikiwa na MP 16 na nyingine ina MP 24.

simu ya kwanza yenye RAM GB 8

Kwa uraibu wa kupiga picha kamera ya kwenye simu hii inaweza ikasababisha uraibu ukaongezeka mara dufu.

Memori ya ndani/Bei. Honor 10 GT ina diski uhifadhi wenye ukubwa wa GB 128; memori ambayo inaweza kubeba vitu lukuki na wala usihisi kama simu imezidiwa uwezo kutokana na kuwa na vitu vingi. Ingawa bei yake haijawekwa wazi lakini inategemewa kugharimu zaidi ya $390|Tsh. 897,000

Mengineyo kuhusu Honor 10 GT.

Inatumia mfumo endeshi wa Android 8.1, USB Type-C, uwazi mdogo (3.5mm) kwa ajili ya spika za masikioni na inatumia kadi mbili za simu pamoja na kushika mawasiliano ya mpaka 4G LTE.

simu ya kwanza yenye RAM GB 8

Kuna kamera ndogo (1.8-micron pixel) kwa mbele kwa ajili ya kuchukua picha/video nzuri sana za kujipiga mwenyewe.

Kiujumla Honor na Huawei wameingia kwenye vitabu kwa kuwa na simu ya kwanza kabisa kuwa na kiwango kikubwa kabisa kwenye RAM. Upatikanaji wake kwa ulimwengu wote bado haujafahamika.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.