fbpx

Huawei na 6G: Tayari utafiti wa teknolojia ya 6G waanza

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Huawei na 6G. Wakati ata bado 5G haijaanza kusambaa sana tayari kampuni ya Huawei imeanza utafiti wa teknolojia ya 6G.

Kampuni ya Huawei tayari imezipiku kampuni nyingi duniani katika uwekezaji na utengenezaji wa teknolojia na vifaa vya mawasiliano vya 5G vyenye ufanisi mzuri na pia kwa bei nafuu kuliko makampuni mengine mengi duniani.

huawei na 6g

Huawei na 6G: Utafiti wa teknolojia hiyo unafanyika nchini Kanada, hii ikiwa ni moja ya nchi ambayo inaweza kuzuia utumikaji wa vifaa vya teknolojia ya 5G vya Huawei kwenye mitandao yake ya simu.

Watafiti wengi wanaamini itachukua zaidi ya miaka miwili teknolojia ya 5G kusambaa na kutumika sehemu nyingi duniani kote, lakini hilo haliwafanya Huawei wasimame. Huawei hawataki kulala na inasemekana tayari wameanza utafiti wa kuja na teknolojia ya 6G umeanza kupitia kitengo chao cha utafiti (R&D) kilichopo jijini Ottawa nchini Kanada.

INAYOHUSIANA  BarraCuda Pro: Diski uhifadhi ya ukubwa wa TB 12 kwa ajili ya kompyuta za mezani

Kwa makadirio ya haraka teknolojia hiyo itaanza kupatikana kwenye miaka ya 2030.

Mafanikio ya Huawei kwenye teknolojia ya 5G yameipa Marekani wakati mgumu kwani makampuni ya nchini humo na pamoja ya mataifa mengine ya magharibi bado hayajafikia kiwango cha ubora na unafuu wa teknolojia na bidhaa za 5G ukilinganisha na Huawei. Huawei kuwa kampuni ya kutoka nchini China linawapa wakati mgumu na hivi karibuni kumekuwa na jitihada kadhaa zinazoonesha harakati za Marekani kujaribu kufanya mataifa rafiki kutonunua vifaa vya teknolojia ya 5G kutoka Huawei.

INAYOHUSIANA  Simu mpya ya BlackBerry, ifahamu BlackBerry KEYone! #2017

Je kwa haraka haraka unadhani itachukua miaka mingapi teknolojia ya 5G kufika katika mataifa yetu?

Chanzo: The Logic
Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.