Huawei Mate XT. Siku ileile ambayo Apple ilizindua simu za iPhone 16, Huawei ilizindua simu yake inayosubiriwa kwa hamu, Mate XT — simu ya kwanza yenye uwezo wa kupinda mara tatu ambayo imetengenezwa kwa wingi na itaanza kupatikana kwa watu hivi karibuni.
Ikiwa ni ya kwanza ya aina yake kwenye soko, Mate XT inauzwa kuanzia $2,810, takribani Tsh 7,100,000, na kuifanya kuwa simu ya gharama kubwa zaidi katika historia ya Huawei.
Vipimo Muhimu vya Huawei Mate XT:
- Kioo: Skrini yenye ukubwa wa inchi 10.2
- Unene: 3.6 mm ikiwa imekunjuliwa kikamilifu
- Betri: Betri lenye uwezo wa 5,600mAh, ikiwa na uwezo wa kuchaji kwa waya au bila waya (wireless charging)
- Kamera: Mfumo wa kamera tatu, ikiwa na sensa kuu ya 50MP, lenzi ya ultra-wide ya 12MP, na lenzi ya telephoto ya 12MP
Bei:
Toleo la 256GB: $2,810, takribani Tsh 7,100,000/=
Toleo la 512GB: $3,092, takribani Tsh 7,800,000/=
Toleo la 1TB: $3,372, takribani Tsh 8,500,000/=
Vipengele Vinavyovutia:
- Njia za Kutumia: Unaweza kuitumia Skrini moja (kama simu ya kawaida), skrini mbili, na skrini tatu (hii ni ukubwa kama wa tableti).
- Matumizi ya Ofisini: Kinanda cha kugusa kinachokunjika kwa matumizi kama kompyuta, keyboard
Kwa Nini Ni Muhimu:
Uzinduzi wa bidhaa za Huawei na Apple kila Septemba umekuwa ni muda muhimu wa kuona ubunifu unaoendelea kwenye teknolojia za simu. Mate XT ya Huawei imetambulishwa na kuonesha ni namna gani kampuni ya Huawei imekuwa na kasi kubwa ya kiubunifu kuizidi Apple. Simu hii mpya ni simu ya kwanza ya teknolojia hiyo kuanza kuuzika, ikiweka alama mpya kwenye soko la simu zinazokunjika. Licha ya juhudi za awali za kampuni kama Samsung, Transsion (Watengenezaji wa Tecno na Infinix), na TCL, Huawei ndiyo ya kwanza kuleta toleo la mkunjo wa mara tatu linalozalishwa kwa wingi, na kufanikiwa kukabiliana na changamoto kubwa za zinazohusisha uzalishaji wake.
Simu hii ya teknolojia ya hali ya juu ni ishara ya ubunifu, ikisukuma mipaka ya kile kinachowezekana kwenye simu zinazokunjika. Hadi sasa tayari watu zaidi ya milioni 2 wameshajiorodhesha katika kuinunua itakapoanza kupatikana (preorder).
Vyanzo: HuaweiCentral na vyanzo mbalimbali
No Comment! Be the first one.