fbpx

Simu za Huawei kukosa apps za Facebook, WhatsApp na Instagram

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kikwazo cha serikali ya Marekani dhidi ya Huawei kinaonekana kuzidi kuisumbua kampuni hiyo. Simu mpya za Huawei kukosa apps za Facebook, WhatsApp na Instagram kutokana na Facebook kuitikia wito wa serikali yao.

huawei

Hichi ni moja ya kipindi kigumu sana kwa Huawei kibiashara

Makampuni ya utengenezaji simu kama vile Huawei huwa yanapata malipo kadhaa kwa kila simu inayouzwa ikiwa na app kutoka makampuni kama vile ya Facebook, Booking.com au Twitter. Biashara za mtandao nyingi zinatambua umuhimu wa apps zao kuja moja kwa moja kwenye simu mpya.

INAYOHUSIANA  App ya kujitegemea ya Instagram Direct kuondolewa!

Facebook wameipa notisi Huawei wakitaka simu zozote kuanzia sasa ambazo zinatoka kwenye viwanda vya kampuni ya Huawei kutokuwa na apps zake za aina yeyote – apps zinazomilikiwa na Facebook Inc ni pamoja na Facebook, Messenger, WhatsApp, Instagram na Boomerang.

Facebook wameungana na kampuni ya Google katika kufuata katazo lililotolewa na serikali ya Marekani dhidi ya kampuni ya Huawei. Serikali ya nchi hiyo imeiingiza kampuni ya Huawei kwenye orodha ya makampuni ambayo si mwananchi wala kampuni ya kimarekani inatakiwa kufanya nayo mauzo/biashara ya aina yeyote.

INAYOHUSIANA  Fahamu Kwa nini Facebook Inatumia Rangi Ya Bluu!

Kwa wanaotumia simu za Huawei kwa sasa hawataathirika, pia simu ambazo zishaingia kwenye maduka pia zitafanya kazi kama kawaida.

Huawei kukosa apps za Facebook

Huawei kukosa apps za Facebook:Kwa sasa bado haijafahamika Huawei watachukua hatua gani kurahisisha upatikanaji wa apps hizo kwenye simu zao

Ila pia tukumbuke ya kwamba simu zinazotoka kiwandani kwa sasa pia zitaanza kutokuja na soko la Google Playstore, na hili likishaanza kutokoa itakuwa vigumu sana kwa Huawei kuvutia watu kwenye simu zao.

INAYOHUSIANA  Unapigiwa simu za usumbufu na matangazo? Google waja na App ya kuzuia

Tayari mauzo ya simu hizo barani Ulaya na katika baadhi ya nchi za Asia yameanza kuathirika – tafiti kadhaa zinaonesha wanunuaji simu mpya wamekuwa na wasiwasi katika kuchagua simu za Huawei kwa sasa.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.