fbpx

Hoteli ya kwanza ya juu ya Anga kufunguliwa mwaka 2022

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kampuni ya Marekani ya Orion Span Inc ya imetangaza mpango wa kujenga hoteli ya kwanza ya anga ya juu iitwayo ‘Stesheni ya Aurora’.

Mpango huo bado uko kwenye kipindi cha kukusanya uwekezaji, lakini sasa watu wanaweza kuweka nafasi safari ya kwenda hoteli hii kwa kulipa dola za kimarekani elfu 80 kama amana ya kwanza.

Hoteli hii itakuwa na vitengo kadhaa ambavyo kila kimoja kina urefu wa mita 13 na upana wa mita 4; ukubwa wa vyumba vya hoteli hii utakuwa karibu sawa na ukubwa wa ndege aina ya Gulfstream G550.

juu ya anga

Hoteli hii itaweza kupokea watalii wanne na wafanyakazi wawili kwa wakati mmoja.

Nnini ambacho watalii watakuwa wanakifanya kwenye hoteli ya angani?

Habari zinasema kwenye hoteli hii watalii watapata kuishi kama wanaanga, kuhisi ukosefu wa nguvu za mvutano wa dunia, kupiga picha ya dunia. Gharama ya kulala kwa siku 12 ni  $9.5m|Tsh 21,375bn.

Vilevile, watalii hao wataweza kufanya majaribio ya kisayansi, kupanda mboga, kutazama mwanga aina ya Aurora na kutazama Mawio na Machweo kwa zaidi ya mara 10 ndani ya siku moja. Lakini kabla ya kwenda hoteli hii, watalii watahitaji kupata mafunzo kwa miezi mitatu.

juu ya anga

Hoteli hii itasafiri kwenye mzingo ulioko kilomita 320 juu ya Dunia na kuzunguka mzingo mmoja kila baada ya dakika 90.

Sayansi na teknolojia ndio hiyo. Siku zote ulijua tu hoteli zinajengwa ardhini, katika miaka ya hivi karibuni tunafahamu kuwa ipo hoteli iliyojengwa chini ya maji na sasa ni angani. Sijui tunaweza tukaishukuru teknolojia/sayansi, majibu unayo wewe.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Google kuendelea kushirikiana na Huawei kwa siku 90 zijazo
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.