Kila leo kuna simu mpya/toleo jipya la simu linatoka likilenga wateja mbalimbali. HMD Global ambao ndio wanamiliki bidhaa zinazobeba jina la Nokia hivi karibuni wametoa rununu ambazo si ghali.
 Tunafahamu vyema kuna simu nyingi tuu za Nokia sokoni huku zikiwa na bei tofauti tofauti. Kwa wale ambao tunaona simu janja haiwezi kuhimili matumizi yetu ya kila siku hivyo basi kuamua kuwa na “Simu ndogo” (simu za bei rahisi) sina shaka wapo ambao wamenunua rununu za aina hiyo.
Sasa basi HMD Global wametoa simu za bri rahisi-Nokia 105 na Nokia 220 4G. Rununu zote mbili zina uwezo wa kawaida ingawa zinazidiana kidgo.
Nokia 105
Tunaotumia simu ndogo mara nyingi huwa tunaangalia uwezo wa kifaa husika kwenye utunzaji wa chaji, namba za simu zinazoweza kuhifadhiwa tukienda mbali zaidi tunapenda kujua idadi ambayo rununu husika inaweza ikatunza. Nokia 105 ina sifa zifuatazo:-
Uwezo wa betri: 800mAh na linaweza kutoka
Memori: Ina uwezo wa kutunza namba za simu elfu mbili (2,000), jumbe za maandishi mia tano kwa idadi
Laini za simu: Ina sehemu mbili za kuweka kadi za simu
Mengineyo: Ina redio, inachajiwa kwa USB (1.0), tochi ya mwanga ang’avu (LED), sehemu ya kuchomeka spika za masikioni, rangi-Bluu, Udhurungi na Nyeusi.
Bei: $14|Tsh. 32,760 (bei ya ughaibuni)
Nokia 220 4G
Moja ya kitu ambacho kinaipa simu ambazo uwezo wake ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida basi ni kuwa na uwezo wa kuperuzi kwenye intaneti na hapa namaanisha rununu husika kuwa na kivinjari kama moja ya programu zilizomo ndani yake. Mbali na hilo sNokia 220 4G ina sifa zifuatazo:-
Uwezo wa betri: 1200mAh na linaweza kutoka. Ina uwezo wa kukaa na umeme kwa siku 27, inaruhusu mtu kuitumia kwa kuongea tu mpaka saa sita (6).
Kamera: Ina kamera moja+uwezo wa kupiga picha zenye ung’avu (flash)
Intaneti: Inatumia 2G na 4G
Laini za simu: Ina sehemu mbili za kuweka kadi za simu
Mengineyo: Ina redio, bluetooth 4.2, USB (2.0), tochi ya mwanga ang’avu (LED), sehemu ya kuchomeka spika za masikioni, rangi-Bluu na Nyeusi
Bei: $43|Tsh. 100,620 (bei ya ughaibuni)
Simu zote mbili zimechambuliwa kwa mapana yake sasa ni wewe kuamua ipi imekuvutia na pengine kufanya mipango ya kuweza kuinunua. Sisi kazi yetu tunaleta mbele yenu halafu wewe mwenyewe unafanya maamuzi.
Vyanzo: GSMArena, Gadgets360