fbpx

Hisa za Jumia zaporomoka katika soko la hisa la New York

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Hisa za Jumia zaporomoka katika soko la hisa la New York nchini Marekani. Hali hiyo ambayo haijawashangaza baadhi ya watafiti, hisa za kampuni hiyo zaporomoka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na kipindi cha mwanzoni cha kuanza kuuzwa – Aprili.

hisa za jumia

Kwa watu walionunua hisa kipindi kampuni hiyo imeuza hisa zake kwa mara ya kwanza basi hisa zao zinathamani ya nusu ya thamani ya mwanzo: kwa sasa hisa zake zinauzwa kwa kati ya dola 7.56 hadi 8.73, wakati hisa zimeanza kuuzwa ziliuzwa kwa dola 14.50 mwezi wa nne mwaka huu.

INAYOHUSIANA  Kufuta Meseji WhatsApp: Sasa ni rasmi kwa watumiaji wa app hii maarufu

Hisa zilivyoanza kuuzwa kuna muda thamani ya hisa za kampuni hiyo zilipanda hadi kufikia dola 49.77 – bei hii ilifanya kampuni hiyo kuwa na thamani ya dola bilioni 4 za Kimarekani katika soko la hisa. Kwa sasaa kwa bei ya dola 7.93 inaliweka kwenye thamani ya dola milioni 614.9 tuu.

Hisa za Jumia

Muda baada ya kuanza kuuza hisa zake katika soko hilo maarufu duniani kuna shutuma zilitolewa kuhusu kampuni hiyo kutumia data zisizo za kweli kuvutia wawekezaji, wenyewe walipinga hili.

INAYOHUSIANA  Rasmi Apple yainunua App ya Shazam kwa bilioni 897.58

Watafiti wana mtazamo ya kwamba kwa bei ya hisa za mwanzo kampuni hii ilipewa thamani kubwa kuliko uhalisia na hali hii inayoonekana sasa ndio thamani halisi ya kampuni hii – na tusishangae ikishuka zaidi kutokana na changamoto zilizopo katika huduma za Jumia barani Afrika.

Vyanzp: Quartz na tovuti mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.