fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

simu Uchambuzi

Hii ndio Samsung Galaxy Note 8! #Uchambuzi

Hii ndio Samsung Galaxy Note 8! #Uchambuzi

Spread the love

Jijini New York, Kampuni ya Samsung imezindua simu yake ya Note 8 ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa baada ya anguko la Note 7 iliyopatwa na matatizo ya betri yake kusababisha kuungua kwa simu.

Hatua hii inakuja baada ya kampuni ya Samsung kupata msukosuko wa kibiashara ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu ilipotoa simu ya Galaxy note 7 ambayo betri zake zilikuwa zinalipuka hivyo kulazimika kutolewa sokoni.

Samsung Note 8 imekuja na ongezeko la ukubwa wa kioo chake kwa inchi 6.3 chenye teknolojia ya Super AMLED curved Infinity Display (Uwiano (ratio – 18.5:9)

Ongezeko hili la kioo ni la ukubwa wa nchi 0.1 ikilinganishwa toleo la S 8.

samsung galaxy note 8

Samsung Galaxy Note 8: Kwa wale walionunua toleo la Note 7 lililopatwa na skendo ya milipuko ya moto wanapewa punguzo kubwa la bei pale watakapoweka oda za Note 8

Pia washabiki wa simu za Samsung za familia ya Note watapata S Pen yenye uwezo bora zaidi, ambapo sasa unaweza kutumia kalamu hiyo maaalum hata pale kioo kikiwa kimezima.

SOMA PIA  Utafiti: Watumiaji wa iPhone huwa 'hawawapendi' kimapenzi watumiaji wa Android

Yaani Samsung wameongeza kipengele kinachoitwa `Screen Off Memo` ambacho unaweza kutoa S Pen yako na ukaweza kuandika kitu chochote kwenye kioo na kukihifadhi bila ya kuwasha Skrini yako.

samsung note 8

Kamera mbili za nyuma

katika toleo hili jipya la simu ya Galaxy note 8 imekuja na vitu vipya katika teknolojia ya usalama, ambapo ina uwezo kutambua muonekano wa mmiliki wa simu, alama za vidole, mboni ya jicho na mfumo mpya wa kiusalama ujulikanao kama Samsung Bixby ambayo inatoa sauti maalumu za maelekezo ya kuweka ulinzi wa siri wa simu hiyo ubora mpya wa picha.

SOMA PIA  Ifahamu Tecno Camon CX (Toleo La Manchester City), Sifa Na Uwezo! #Uchambuzi

Sifa za simu hiyo ni kama ifuatavyo

  • Kamera ya mbele– 8MP
  • Kamera ya nyuma– zipo mbili zenye 12MP
  • Ukubwa wa uhifadhi wa ndani– 64GB
  • Mfumo Endeshi– Android 7.0 Nougat
  • Ukubwa wa RAM– 6GB
  • Prosesa– Samsung Exynos 8895
  • Ukubwa wa kioo– Inchi 6.3
  • Uwezo wa Betri- 3,300-mAh
  • Mfumo wa Ulinzi– Iris scanner/Fingerprint Scanner
Samsung Galaxy Note 8

Samsung Galaxy Note 8: Mwaka huu Samsung wanaamini majanga ya moto wa toleo la Note 7 ni historia tu kwa sasa.

Simu hiyo tayari unaweza kuweka oda yako na bei inakadiriwa kuwa zaidi ya Tsh 2,400,000/=. Tutakuletea taarifa zaidi kuhusu toleo hili la Samsing Galaxy Note 8, endelea kutembelea Teknokona.

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania