fbpx

Halotel Tanzania kuwekeza zaidi

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Katika biashara kuna njia nyingi za kujidhatiti lakini kitu kimoja ambacho kamwe hakipaswi kusahaulika ni kuwekeza zaidi ili kutanua wigo wa biashara na kuwafikia watu wengi zaidi.

Halotel Tanzania kampuni ambayo haina hata miaka mitano tangu kuanza kufanya kazi imepanga kuongeza nguvu kwenye uwekezaji ambao umekuwepo tayari na matunda yake yakionekana.

Mwezi Oktoba 2018 Halotel Tanzania imetimiza miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake na kuweka wazi kuwa itaongeza $200 milioni kwenye uwekezaji wake ambao kwa jumla utafikia $700 milioni.

Nafasi ya Halotel kiushindani na uwekezaji.

Halotel ambayo ndio kampuni kinara kwa kuwa na miundombinu maeneo mengi nchini Tanzania wamekuwa wakidhatiti kwa kuendelea kuwepo kwenye nafasi tatu (3) bora kwenye ushindani. Kufahamu zaidi>>BOFYA HAPA.

Kwenye uwekezaji huo ambao unafikia nyongeza ya $200 unamaanisha kuwa Halotel Tanzania kuwafikia wateja mil. 6 katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Mbali na hapo Halotel inaendelea kuboresha huduma za HaloPesa, teknolojia ya mawasiliano kwa ajili ya mashirika na serikali kwa ujumla.

Halotel Tanzania

Miundombinu ya Halotel Tanzania ambayo inawafikai wananchi kwa 95%.

Tusubiri tuweze kuona matokeo ya kuongezwa kwa uwekezaji ambao kiujumla unalenga kuimarisha yale ambayo yamekuwepo kwa miaka mitatu sasa.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Usajili wa kadi za simu kwa njia ya alama za Vidole mwisho ni Disemba 31 mwaka huu
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.