Je wewe unakipaji cha uandishi wa stori mbalimbali? Au ni mpenzi wa kusoma stori mbalimbali? Basi Hadithi app ni app ya kudownload.
Ni app ya kitofauti sana na uwezi kubisha ya kwamba ni app yenye umuhimu kwa watu wote wanaopenda kusoma hadithi (stori) za kiswahili, na waandishi pia – kwani kupitia app hii wote wawili (watunzi na wasomaji) wanaunganishwa kwa urahisi sana.

Nimeitumia app hii kwa zaidi ya wiki 3 sasa na huu ndio mtanzamo wangu;
- Waandishi wanazidi kuongezeka na stori mpya pamoja na miendelezo inaendelea kuwekwa.
- Na nimependa kuona kukiwa na stori mpya n.k unapata taarifa kupitia eneo la ‘notification’
- Ni app isiyo na muda mrefu sana ila inaonekana tayari imepata wasomaji wengi kwani kupitia data zinazoonekana kwenye kila stori – imetazamwa mara ngapi – zinaonesha watu wanazisoma hadithi sana
Mara unapoifungua unakutana na eneo linalokuonesha Stori Mpya, chaguo la pili ni Makundi (yaani aina za stori), na mwisho ni waandishi.
Stori katika app hii zimegawanywa katika makundi ya;
- Maisha
- Mapenzi
- Chombezo
- Upelelezi
- Uchawi
- Mapigano
- Vichekesho
Lakini katika muda mdogo niliotumia naona stori za mapenzi ndio zinapendwa zaidi na wasomaji…. 🙂
App hii kwa sasa inapatikana katika soko la Google Play | Hadithi App , ipakue na utuambie mtazamo wako juu ya app hii kwenye eneo letu la comment.Â
One Comment
Comments are closed.