Mfanyabiasha mmoja mwenye asili ya Uchina amehukumiwa kwenda jela miaka minne kwa kosa la kujihusisha na kudua mtandao wa ndege (Boeing) iliyochini ya Jeshi la Marekani.
Mfanyabiashara huyo alikiri kosa la kujihusisha na kupata taarifa mbalimbali kutoka kwenye mtandao wa ndege aina ya Boeing pamoja na vitu vingine ambavyo ni muhimu kwa jeshi la Marekani.
Bw. Stephen Su alikuwa ni mmoja wa watu walioshiriki kuiba taarifa mbalimbali zilizojumuisha data kuhusu ndege aina ya C-17 and utumiaji ndege za kivita aina ya F22 na F35.

Inasemekana mfanyabiashara huyo alitoa msaada kwa wadukuzi hao kutoka jeshi la Uchina kuweza kufanikisha lengo lao. Serikali ya Uchina imekanusha madai hayo ya kuhusika katika udukuzi wa taarifa mbalimbali kutoka Jeshi la Marekani.

Bw. Su na wenzake wawili walikuwa na mpango wa kuziuza taarifa hizo kwa makampuni nchini China kwa ajili ya kuinua uchumi wa Uchina. Kazi ya mfanyabiashara huyo ni kusema data gani za kuchukua baada ya kufanikiwa kudukua na kuona taarifa mbalimbali.
Katika harakati za kudukua mfanya biashara huyo na wenzake wawili walitengeneza ripoti kuhusu data walizozichukua na taarifa gani zitakuwa na faida kwa makampuni waliyokuwa wamepaga kuwauzia data hizo kutoka Jeshi la Marekani. Hata hivyo taarifa hiyo ilikamatwa na mamlaka husika za Marekani.
Je, hatua hiyo ya mfanyabiashara huyo kuhukumiwa kifungo cha jela kitazidisha mahusiano kati ya Uchina na Marekani? Endelea kusoma makala mbalimbali ili na wewe uhabarike kupitia TeknoKona.
Vyanzo: Tech Times, The Verge