fbpx
apps, Google, Play Store

Google Yazuia App Zinazouza Mihadarati (Bangi) PlayStore!

google-yazuia-mihadarati-bangi-playstore
Sambaza

Ndio kuna App zimekua zikifanya biashara ya kuuza mihadarati (bangi) katika mtandao kwa muda mrefu tuu na Google wameliaona hilo na sasa wamechukua hatua.

Hatua hii ya kuzitoa App hizo imefika baada ya Google yenyewe kubadilisha vigezo na masharti ya PlayStore. Watu wenye App hizo wanalazimika kutoa kipengele cha kusambaza (delivery) ya mihadarati hiyo.

Mmea Wa Mihadarati (Bangi) Ukiwa Shambani
Mmea Wa Mihadarati (Bangi) Ukiwa Shambani

Kama wakishindwa kabisa kusitisha huduma ya usambazaji basi inawaladhimu Google wenyewe kufuta App hiyo katika soko lao.

INAYOHUSIANA  Uber kufanya Majaribio magari Yanayojiendesha yenyewe

Google wamefikia uamuzi huu na katu hawajali hata kama matumizi ya mihadarati yameruhusiwa katika sehemu husika, kwa mfano kuna baadhi ya nchi au maeno ambapo matumizi ya mihadarati yameruhusiwa, lakini Google hawajali hilo.

“Haturuhusu App ambazo zinarahisisha uuzaji na ununuzi wa mihadarati au bidhaa za moihadarati” — Google

Moja Ya Tangazo La App Ambayo Inatumika Katika Kusambaza Mihadarati (Bangi)
Moja Ya Tangazo La App (Eaze) Ambayo Inatumika Katika Kusambaza Mihadarati (Bangi)

Hii imetokea baada ya PlayStore kuongeza au kuboresha vitu ambavyo haviruhusiwi katika soko lao. Hivyo basi App zote zinazojihusisha na jambo hili inabidi kutoa kipengele hicho cha kununua mtandaoni.

INAYOHUSIANA  Jinsi Ya Kutoa Namba Yako Ya Simu Katika Hifadhi Ya TrueCaller!

Wenye App hizo wamepewa mwezi mmoja tuu ili kuendana na tamko hilo, wote ambao watashindwa kufanya hivyo swala ni kwamba App zao zinaweza hata kufungiwa kabisa.

Tuambie wewe unaonaje uamuzi ambao umefikiwa na kampuni ya Google katika swala hili? niandikie hapo chini katika sehemu ya maoni. ningependa kusikia kutoka kwako.

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia.!

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com