Ni wazi kuwa chapa ya Pixel imejipatia jina kubwa sana na inamilikiwa na kampuni ya Google, kwa upande wake wa simu chapa inafanya vizuri sana.
Vipi kwa upande wa Laptop? Kwa habari ambazo zinasambaa sasa ni kwamba kampuni imeachana kabisa na mpango wake wa kuzalisha kompyuta ambazo zingejulikana kama Pixelbook.

Kingine ni kwamba kampuni haijaachana na mpango huo tuu, mpaka ile timu nzima ambayo ilikua imepewa au ingepewa jukumu hilo imeshambaratishwa.
Hapo unaweza kujiuliza mbona Google wamefikia hatua hiyo ambayo wengi hawajaidhania kabisa, kingine cha kujua ni kwamba timu hiyo ilishatoa laptop hapo nyuma.
Kwa sasa Pixelbook Go ndio itakua laptop ya mwisho kabisa kutoka katika timu hiyo maana wanaachana kabisa na utengenezaji wa matoleo ya mbele.
Kingine ni kwamba kama kila kitu kingekua sawa ni kwamba toleo jipya (baada ya Pixelbook Go) pengine lingetoka mwakani.
Hivi karibuni kampuni ya Google imekua ikiweka wazi kuwa itapunguza baadhi ya nguvu kazi katika kampuni (mfano, wafanya kazi), kupunguza kasi ya kuajiri nguvu kazi na vile vile kauchana kabisa na baadhi ya bidhaa/biashara.
Google imeweka wazi kuwa mpango wake kupitia bidhaa zake za Pixel, ni kwamba mpango wake ni kutengeneza bidhaa nzuri na kisha hata kuwapa somo wapinzani jinsi ya kufanya hilo.
Ikumbukwe kwamba ambacho kipo wazi mpaka sasa ni kwamba kampuni imeachana kabisa na uzalishaji wa matoleo mapya kwa bidhaa hiyo kisa kikubwa kikiwa ni sababu za kiuchuni
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani ni sawa kwa makampuni haya kuendelea kupunguza baadhi ya bidhaa/biashara na wafanya kazi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.