fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Google Google Pixels simu Uchambuzi

Google Pixels 6 – Google kupitia prosesa yao waleta simu bora kwa bei nafuu

Google Pixels 6 – Google kupitia prosesa yao waleta simu bora kwa bei nafuu
Spread the love

Google Pixels 6 na 6 Pro ni simu janja mpya zilizotambulishwa na Google na zitaanza kupatikana kama toleo la kufunga mwaka huu kutoka kwao. Hizi ndio simu za kwanza kutumia prosesa ya Google Tensor, matoleo ya nyuma yalikuwa yanatumia prosesa za Snapdragon.

Kwa kutumia prosesa yao Google wanahakikisha mifumo ya kiteknolojia ya huduma za Google, utumiaji wa chaji na ata uwezo wa teknolojia za AI unakuwa bora zaidi kuliko kutegemea chip kutoka kwa watengenezaji wengine. Kwa sasa wanauwezo wa kutengeneza na kufanya maboresho ya Android na kuboresha chip zao ili kukidhi mahitaji ya matoleo yao ya Android – hili ndilo jambo lililochangia sana mafanikio ya simu za iPhone zinazotolewa na Apple.

pixels 6 google

Simu ya Google Pixels 6 Pro na Pixels 6

Hii ni simu yenye moja ya kamera bora zaidi kwa mwaka huu kwa simu janja

 

SOMA PIA  Uchambuzi wa Tecno Spark 5, Uwezo na Sifa.

Kupitia simu hizi Google analeta ushindani mkubwa hasa wa kibei kati ya matoleo haya na matoleo ya simu zenye uwezo na sifa kama hizi kutoka makampuni ya Samsung, Apple na wengine.

Google Pixels 6 inapatikana kuanzia kwa $599 (Takribani Tsh 1,400,000/=) wakati toleo la Pixels 6 Pro linaanza kwa $899 (Takribani Tsh 2,100,000/=).

Sifa ya Google Pixels 6

simu pixels 6 google

Pixels 6

 • Programu Endeshaji: Android 12
 • Display: 6.4 inchi (1080p, 90Hz, OLED)
 • Kamera:
  • Kamera kuu – Megapixel 50-megapixel, pia kuna kamera spesheli ya upana mkubwa (ultrawide) ya megapixel 12(uwezo wa kuona nyuzi 114 ya eneo)
  • Kamera ya Selfi: Megapixel 8
 • Prosesa: Google Tensor chipset
 • RAM GB 8, Diski Uhifadhi GB 128 na 256
 • Teknolojia zingine: Wi-Fi 6E, Bluetooth 5.2, 5G kwenye mfumo wa mmWave, kuchaji bila waya (Wireless charging)
 • Ports: USB-C
 • Uwezo wa Betri: mAh 4614

Pia zimekuwa simu za kwanza kutoka Google pia port ya kutumia earphone (audio jack), pia haziuzwi na chaja. Makampuni mengi yanaanza kutokuweka chaja kwenye mauzo ya simu mpya kutokana na imani ya kwamba watumiaji wengi tayari wana chaja nyingi za simu zao zingine – hivyo ni uamuzi bora katika kulinga mazingira.

Sifa ya Google Pixels 6 Pro

Pixels 6 Pro

 • Programu Endeshaji: Android 12
 • Display: 6.7 inchi (1440p, 120Hz, OLED)
 • Kamera:
  • Kamera kuu – Megapixel 50-megapixel, pia kuna kamera spesheli ya upana mkubwa (ultrawide) ya megapixel 12 (uwezo wa kuona nyuzi 114 ya eneo), na kamera ya uwezo wa kuzoom zaidi (telephoto lens) x4
  • Kamera ya Selfi: Megapixel 11.1
 • Prosesa: Google Tensor chipset
 • RAM GB 12, Diski Uhifadhi GB 128, 256 na GB 512
 • Teknolojia zingine: Wi-Fi 6E, Bluetooth 5.2, 5G kwenye mfumo wa mmWave, kuchaji bila waya (Wireless charging)
 • Ports: USB-C
 • Uwezo wa Betri: mAh 5004
SOMA PIA  Facebook Pages: Kuonekana/kutoonekana kwa ukurasa

Tayari watu washaanza kufanya malipo (preorder) ila simu hizi zitaanza kuingia sokoni kuanzia 28 Oktoba mwaka huu.

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania