fbpx
Android, apps, iOS, Teknolojia

Google One inapatikana BURE kwenye iOS na Android

google-one-inapatikana-bure-kwenye-ios-na-android

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Si bidhaa nyingi za Google ambazo zinapatikana/zinaweza kutumika kwenye iOS na hivi sasa wenye simu janja zinazotumia Android ama iOS wataweza kupata huduma ya Google One.

Kutokana na ukuaji wa teknolojia katika dunia ya leo si kitu cha ajabu kwa mtu kuhifadhi vitu mbalimbali sehemu ambayo haiwezi kufikika kirahisi na kuweza kuweza kupata huduma muda wowote sehemu yoyote.

Google One ni nini?. Hii ni huduma inayomuwezesha mtumiaji wa kifaa cha kidijiti kuweza kuhifadhi vitu vyake sehemu ambayo ataweza kuweka/kutoa nyaraka/vitu mbalimbali muda wowote atakaotaka.

Google One
Programu tumishi ambayo ni memori ya zida iliyoanzishwa mwaka 2018 na ilipatikana kwenye Android pekee.

Huduma hii haina tofauti sana na GDrive, Google Photos, iCloud, OneDrive ingawa hapo awaali mtumiaji wake ilibidi ajisajili (kulipa ada kidogo) kuweza kupata huduma lakini hivi sasa ni BURE ambapo mtu atajisajili kwa barua pepe ya Gmail nas kupewa GB 15 (haziuzwi) za kutunza vitu vyake ingawa mtu anaweza akalipia $1.99 kwa mwezi kuweza kupata GB 100 au zaidi ya hapo kulingana na utakachohitaji.

INAYOHUSIANA  Solar Paper: Hii Inachaji Simu Janja Kwa Masaa Mawili Na Nusu Tuu!

Hii programu tumishi sasa inapatikana kwenye Playstore. Upande wa iOS inaelezwa kuanza kupatikana hivi karibuni. Tuambie habari hii imekufurahisha ukiwa kama mtu ambae unapenda kuhifadhi vitu “Kusikojulikana?”

Usisite kutufuatilia kila leo kwa habari mbalimbali zinazohusu teknolojia.

Chanzo: The Verge

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|