fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Apple apps Google Google Pay

Google Kufuta Zaidi Ya App Laki 9 Zilizotelekezwa!

Google Kufuta Zaidi Ya App Laki 9 Zilizotelekezwa!

Spread the love

Ni wazi kuwa katika soko la App la Google Play Store kuna App nyingi sana, katika App hizo kuna zile ambazo zimetelekezwa.

App hizi zinaweza kuwa zimetelekezwa kwa muda mrefu, bila hata ya kupewa sasisho (update) yoyote kwa muda mrefu.

Google Playstoremate 30 pro

Google Playstore

Hii ni hatua nzuri maana kuihalisia soko lina Apps nyingi sana ambazo zinahitaji kupunguzwa. App hizi kwa haraka haraka ni zile ambazo hazijaguswa (kupewa sasisho) kwa kipindi cha miaka miwili au zaidi.

Kwa google namba kamili ya App hizo ni 869,000 ukaichana na Google wao Apple katika soko lao wanapambana na App 650,00 tuu.

Ngoja kwanza hivi hapo juu… nilisema kufuta???????

Kinachofanyika hapa ni kwamba makampuni hayo yanazificha hizi App yaani ukiwa unazitafuta katika soko husika huwezi kuzipata.

SOMA PIA  Connectify Hotspot: Tumia Intaneti Ya Kompyuta Yako Moja Kwa Moja Katika Simu Janja Yako!

Google PlaystoreHili litabadilika mara tuu mwenye App atakafanya sasisho (update) katika App husika, ndipo App hiyo itaanza kupatikana kama kawaida.

Makampuni yanadai kuwa yanafanya hivyo ili kulinda mambo ya kiulinzi na usalama….

Ningependa kusikia kutoka kwako,niandikie hapo chini katika uwanja wa comment hii umeipokeaje?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii

SOMA PIA  Apple Watambulisha iPhone 6S na 6S Plus, Haya Ndiyo ya Kufahamu Kuhusu Simu Hizo Mpya

Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania