Google kupitia mtandao wake wa kijamii wa Youtube umeamua kufifikia vifaa vingi Zaidi vya Apple kupitia huduma ya Picture-In-Picture.
Kumbuka kipengele hichi cha picture-in-picture kilitangazwa rasmi mwaka jana huku kikiwa kinapatikana katika huduma ya Youtube Premium

Kwa sasa kampuni imetangaza kuwa kipengele hichi kwa kupatikana kwa watumiaji wa Youtube Premium na wale wa Youtube ya kawaida.
Watumiaji wa iOS na iPadOS wote wataweza kufurahia huduma hii kwa urahisi kabisa, kinachotakiwa ni kwamba vifaa hivyo inabidi viwe na toleo la iOS 15 au iPad OS 15 na matoleo ya juu Zaidi kuweza kufurahia huduma hii.
Kwa sasa huduma hii itaanza patikana kwa baadhi ya maeno na kisha baadae kupatikana duniani kote.

Picture-In-Picture kutoka yutube ni uwezo wa kutumia huduma ya Youtube huku unafnaya mambo yako mengine
Kwa mfano unaweza ukawa unatumia unaangalia video katika mtandao huo huku unatuma meseji au kucheza gemu kupitia kifaa hicho hicho.
Ili kujua kama unaweza kuanza kutumia kipengele hichi (kama na wewe kimekufikia) nenda katika katika App ya Youtube na kisha nenda katika eneo la Settings
Ingia katika General na kisha ruhusu uwezo wa Picture-In-Picture

Mpaka hapo utakuwa uwezesha huduma hii, lakini kama bado utashindwa kufanya hivyo huna budi kusubiria mpaka toleo likufikie.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je huduma hii ushawahi kuitumia au una shauku sana ya kuanza kuitumia?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.