Google kukuambia kama password yako imedukuliwa! #Extensions

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Je utafahamu vipi kama password yako imedukuliwa? Inaweza ikawa ni kwenye tovuti ya mtandao wa kijamii au tovuti nyingine ya aina yeyote, kila mwaka udukuzi unaohusisha maelfu ya akaunti za mitandaoni hufanyika.

Google wamekuja na extension ya kivinjari cha Chrome kwenye kompyuta ambacho kitakupa taarifa kama akaunti unayotaka kulogin kwa wakati husika imedukuliwa.

Utumiaji wake;

  • Nenda kwenye soko la extensions la Google (Utaweza kuweka kwenye vivinjari vya Chromium, Chrome, Opera na ujio wa Edge mpya inayotumia Chromium).
  • Ukishapakua na kikaa kwenye kivinjari chako basi ndio mwisho wa wewe kuitaji kufanya lolote
  • Pale utakapotembelea tovuti mfano Gmail au Facebook, kitendo cha wewe kulogin muda huo huo extension hiyo itatumia username yako kusearch kwenye maelfu ya data za akaunti ambazo taarifa zake – hasahasa passwords, zimevuja. Kama ni hivyo notification ya kukutaarifu na kukushauri ubadili password/nywila itatokea.
Google kukuambia kama password yako imedukuliwa

Google kukuambia kama password yako imedukuliwa

Kwa sasa inasemekana kuna taarifa za jumla ya data za akaunti bilioni 4 kwenye mfumo ambao extension hiyo itakuwa inachunguza kama akaunti husika imekwishadukuliwa taarifa zake.

INAYOHUSIANA  Fahamu Tofauti ya Kufuta (delete) na Kuzima (deactivate) Akaunti ya Facebook

Google wamesema mfumo mzima wa kuangalia taarifa za kama zimevuja haziusishi uwekaji wa taarifa za passwords/nywila za akaunti ya mtu. Ni mategemeo ya wengi teknolojia hii itakuja kujengewa ndani ya vivinjari katika siku hizo zijazo – bila uhitaji wa kupakua kama extension.

Kwa watumiaji wa vivinjari vya Chrome, Chromium, Opera mnaweza kutembelea soko la extensions kupakua uwezo huu kwenye vivinjari vyenu. – Chrome Soko la Extensions

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.