fbpx

Google kuufunga mtandao wao wa kijamii wa Google Plus

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Google+ inafahamika na watu wengi sana pia ni rahisi kabisa kujua ipo chini ya nani. Pengine huwa unaiona tuu kwenye simu janja yako lakini hujawahi hata siku moja kuitumia.

Inawezekana ikawa sio taarifa nzuri hasa kwa wale ambao tumezoea kuchapisha/kuona machapisho mbalimbali kutoka kwa wale watu tunawafuatulia kwenye Google+ nikikwambia kuwa Google wanasitisha huduma kwenye mtandao huo wa kijamii.

Sababu kwanini Google imefikia uamuzi wa kuifunga kabisa Google Plus.

Kuna makosa yalifanyika kwenye moja ya sehemu ambapo programu zinaandikwa (wanaelewa waandishi wa programu za kompyuta) kitu amabcho kilishababisha watu hao kuweza kusoma taarifa mbalimbali za watu walojiunga kwenye mtandao huo wa kijamii uliopo chini ya Google.

Kitu kibaya zaidi katika udhaifu huo pia iliwezekana kuona taaarifa za watu ambazo hazipo wazi kwa lugha rahisi zipo kwenye kundi ambalo mtu aliamua kuweka faragha.

Karibu taarifa za watu 500,000 zilizojumuisha majina, barua pepe, anuani, kazi, taarifa binafsi kuhusu mahusiano, tarehe ya kuzaliwa na jinsia ziliweza kuonwa na waundaji wa programu.

Google Plus

Google Plus kufungwa kutokana na kosa la kiufundi.

Sasa Google watafunga huduma za Google Plus katika kipindi cha miezi kumi ijayo kutokana na kuonekana kushindwa kukabiliana na udhaifu uliokuwepo tangu mwaka 2015.

Vyanzo: GSMArena, Redmond Pie

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  iTunes Kutokufa Kabisa Katika Windows!
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.