Google kupitia blog yao watambulisha huduma mpya kupitia mtandao inayoitwa AutoDraw.
AutoDraw ni huduma inayotumia teknolojia inayokuja kwa kasi ya utashi wa kompyuta (AI – Artificial Intelligence) kumsaidia mtumiaji kuchora kwa ufanisi zaidi.
Teknolojia inayozipa vifaa vya elektroniki kama vile kompyuta na simu uwezo mkubwa wa kujifunza na kumsaidia mtumiaji wake imekuwa ikikua kwa kasi sana katika miaka hii. Kwa lugha ya kimombo uwezo huo wa kiakili kwa vifaa vya kielektroniki kama kompyuta unatambulika kwa jina la Artificial Intelligence.
AutoDraw inafanyaje kazi?

AutoDraw ina maelfu ya michoro iliyochorwa na wasanii mbalimbali wakubwa wenye vipaji vya uchoraji. Kutumia teknolojia ya Artificial Intelligence mtandao huo utaweza kutambua ni kitu gani unataka kuchora na hivyo kukupatia mapendekezo ya michoro mbalimbali iliyochorwa kwa usahihi zaidi.
- Ukichagua basi mchoro wako unaboreshwa kwa kutumia mchoro kutoka mfumo wa AutoDraw.
Mfano: Kushoto, mchoro uliochorwa na mtumiaji. Kulia, mchoro uliopendekezwa kutumika na AutoDraw - Kupitia kuunganisha michoro mbalimbali utaweza kuchora chochote kile ambacho ungependelea.
- Ukimaliza unaweza kusambaza mtandaoni kwa wengine au unaweza ukadownload katika mfumo wa picha wa PNG.
Kupitia AutoDraw ata mtu mwenye kipaji kidogo sana cha uchoraji ataweza kuchora kwa haraka zaidi na kwa michoro inayovutia zaidi.
Unaweza kutumia huduma hii kupitia tovuti ya AutoDraw (kwa watumiaji wote wa simu na kompyuta) – http://www.autodraw.com/ .