
Ukiachana na kusubiriwa kwa muda mrefu, tamko limetoka rasmi kuwa msaidizi kutoka Google (Google Assistant) atafika katika saa janja maarufu kutoka Google.
Kiongozi wa juu kabisa kutoka Google, Patrick Chomet amesema kuwa kipengele hicho kitawasili katika saa hizo mwaka huu.

Galaxy Watch 4 Series
Unaweza ukajiuliza ni kwanini Samsung wameamua kufanya kazi na Google katika hii lakini kwa majibu yao ni kwamba walitaka waje na kitu bora kabisa.
Lakini kingine kumbuka hili jambo lilikua ni la muda tuu lakini hakuna haikuwa wazi juu ya lini jambo hili litafanyika.

Galaxy Watch 4 Series…
Kumbuka hivi karibuni Google nao wametangaza saa janja yao ambayo inajulikana kama Pixel Watch.
Kwa sasa kuna saa janja nyingi sana kutoka aktika makampuni mbalimbali haswa katika makampuni ya simu.

Galaxy Watch 4 Series….
Hii imekua ni sehemu kwa makampuni hayo ambapo wanajipatia kipato Zaidi licha ya kuwa wanategemea mauzo ya simu zao tuu.
Ningependa kusikia kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment hii umeipokeaje? Na je ushawahi kutumia saa janja.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn