fbpx

Gmail kuja na barua pepe zinazofutika baada ya muda

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Google wanategemea kuja na maboresha makubwa ya kimuonekano na utendaji katika huduma yao ya barua pepe ya Gmail. Moja ya uwezo unaotegemewa ni mtu kuweza kutuma barua pepe zinazofutika baada ya muda flani.

Maboresho ya kimuonekano yanakuja kwenye huduma mbalimbali za Google, hii ikiwa ni pamoja na huduma zingine kama vile Google Calendar, Google Keep, Google Tasks na zinginezo.

gmail barua pepe inayojifuta barua pepe zinazofutika baada ya muda

Muonekano mpya wa huduma ya Gmail katika tovuti ya www.gmail.com / Muonekano kuja hivi karibani pamoja na uwezo wa barua pepe zinazofutika baada ya muda.

Gmail Confidential Mode

Google wameleta kitu kinaitwa ‘confidential mode’ ndani ya huduma ya barua pepe ya Gmail. Kama barua unayotuma ukaichagulia pangilio/setting hii basi barua pepe yako itatumwa ikiwa na sifa kadhaa;

INAYOHUSIANA  Slack imeboresha kitu na kuzidi kuvutia

Mtu atakayeipokea atashindwa kuituma kwa mwingine (forward). kuidownload. wala kucopy vitu vilivyokwenye barua pepe hii.

Mtumaji barua pepe inayokuwa katika mfumo wa ‘confidential mode’ anaweza iwekea tarehe ya kujifuta huko inakoenda (expiration date), pia anaweza kuchagua uwezo wa kufanya barua pepe hiyo isiweze kufunguka hadi umpatie anayeipokea code (itakayotumwa kwako kwa njia ya sms pale mtu atakapotaka kuifungua barua pepe uliyomtumia).

Gmail kuja na barua pepe zinazofutika baada ya muda

Muonekano eneo la kutuma barua pepe

Je itakuwaje kama mtu akiwa anatumia huduma ya Gmail kwa njia zingine nje ya kwenda mtandao wa Gmail au kutumia app ya Gmail?

  • Kama mtu anatumia njia ya kupokea barua pepe zake kwa njia za POP/IMAP/SMTP, akitumiwa barua pepe yenye sifa ya Confidential Mode hataipata barua pepe hiyo kikamilifu, bali atapata ujumbe utakaomtaka kuifungua barua pepe hiyo kwenye kivinjari/browser.
  • Atapokea barua pepe yenye ujumbe unaosema ‘Ujumbe/Barua pepe hii imetumwa kwa njia ya Gmail Confidential Mode, unaweza kuusoma kwa kubofya hapa’
INAYOHUSIANA  Apple kuzibania apps za Facebook na WhatsApp kwenye iPhone

Google wamesema muonekano mpya, ambao tunaamini utakuja na uwezo huu kwa Gmail, utaanza kupatikana kwa baadhi ya watumiaji wake ndani ya wiki chache kuanzia sasa.

Je unadhani wazo hili ni zuri sana? Tupe maoni yako na usisahau kushare makala hii na wengine.

Gmail: www.gmail.com

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.